"Nakuhurumia pamoja na watoto wako!" Zari akemea mwanadada ambaye amekuwa akiingilia maisha yake

Muhtasari

•Mpenzi huyo wa zamani wa Diamond Platnumz ameonekana kukerwa na mwanadada mmoja anayetuhumu kuingilia sana maisha yake na kueneza maneno mengi dhidi yake.

•Zari amesema mwanadada huyo ameshindwa kuangazia maisha yake mwenyewe kiasi cha kwamba hata ameshindwa kulea mtoto wake.

Image: INSTAGRAM// ZARI HASSAN

Siku ya Alhamisi mwanasoshalaiti na mfanyibiashara mashuhuri Zari Hassan ameamka akiwa mwanamke mwenye ghadhabu tele.

Mpenzi huyo wa zamani wa Diamond Platnumz ameonekana kukerwa na mwanadada mmoja anayetuhumu kuingilia sana maisha yake na kueneza maneno mengi dhidi yake.

Zari amemtaja mwanadada kama mtu aliyekosa nuru maishani huku akimshauri atafute kitu cha maana cha kufanya ambacho kitamsaidia kuondoa jina lake akili mwake.

"Wapendwa, kuangazia maisha yako kunakufanya ukue na ung'ae. Kuangazia maisha ya wengine kunafanya usahau mambo yako mwenyewe. Ni wazo langu tu. Kuna kadada kamoja kanajifanya kanaishi Marekani  na ndiko kashamba kafala zaidi. Hivi vitu unaandika kwa gazeti  ni vya kawaida. Wewe unaandika gazeti, unakosa nuru, unakosa kukula.  Umekuwa na ugonjwa wa Zari, utapona kweli wewe. Nakuomba upate hobby kidogo, cheza gofu ili uweze kutoa Zari akilini mwako. Vibabu sio hobby, huo ni umalaya. Pata hobby kidogo mwanadada, punguza stress. Huna nuru, huna mbele wa nyuma kimaisha na mwili. Angalia mimi, nang'aa, naishi maisha yangu inavyofaa na nina raha. Vititi vyako umevyangalia, vinahitaji upasuaji. Miguu pia na pua!" Zari amesema.

Zari amesema mwanadada huyo ameshindwa kuangazia maisha yake mwenyewe kiasi cha kwamba hata ameshindwa kulea mtoto wake.

Mama huyo wa watoto watano ameyakosoa sana matendo ya mwanadada huyo pamoja na watu wanaoamini maneno yake.

"Wewe umekosa matumani kabisa. Nakuhurumia pamoja na watoto wako. Mpaka mtoto wako ako huko Instagram anawashukuru wengine kwa kumlea. Mama unashinda Instagram kutusi watu na kuumia na maisha ya watu. Yule hana la kutwambia. Maisha yako yenyewe yaonyesha. Alafu wote wanaokwamini ni wajinga. Kuna nini ya kusoma kutoka kwake" Zari alisema.

Zari amewashauri watu kutowashwa na pilipili wasiyoila huku akisema kuwa hiyo ndiyo siri ya kujiendeleza kimaisha.