Natamani nishuhudie Diamond akioa-Uncle Shamte

Muhtasari
  • Kulingana naye, hawezi kungoja kuwa shahidi wakati Diamond atafunga pingu za maisha.
Image: INSTAGRAM// DIAMOND PLATNUMZ

Baba wa kambo wa Diamond, Uncle Shamte amefichua kuwa anatamani siku mtoto wake atafunga pingu za maisha.

Kulingana naye, hawezi kungoja kuwa shahidi wakati Diamond atafunga pingu za maisha.

Akizungumza na Global Publishers, Shamte aliongeza kuwa itakuwa ni jambo la furaha tele kuwepo kwenye harusi ya Diamond.

"Furaha itapitiliza. Furaha huwa haijifichi, mtaiona. Mimi binafsi natamani nishuhudie Diamond akioa kwa sababu namjua mwanangu. Napenda nimuone akifanya jambo hilo," Alizungumz Uncle Shamte.

Matamshi yake yanajiri baada ya msanii huyo kuichua kwamba yuko kwenye mahusiano na anafuraha huku akikana kumchumbia msanii mwenzake Zuchu.

"Zuchu ni msanii wangu na somo la kwanza kuja naye red carpet.....amekua sasa. Mara ya kwanza nilimleta hapa mtoto na sahi amekuwa msanii mkubwa so namleta tena…”

Aidha Zuchu alisema kwamba Diaond anamfahamu mpenzi wake.