Diamond Platnumz aeleza uhusiano wake na Zuchu

Muhtasari

•Diamond Platnumz aliwasili kwenye eneo la tamasha hizo wakitumia gari moja na msanii huyo wa kike, Zuchu.

Diamond na Zuchu
Diamond na Zuchu
Image: hisani

Mwanamuziki nguli Naseeb Abdul almaarufu Diamond Platnumz amefunguka na kueleza uhusiano uliopo kati yake na Zuchu.

Kupitia mahojiano na Wasafi Media, Diamond ameeleza uhusiano kati yake na Zuchu ni kama wa mzazi na mtoto wake na kupuuzilia mbali madai yaliyokuwepo kwamba wanachumbiana.

Diamond Platnumz na Zuchu waliwasili kwenye eneo la tamasha la usiku wa Valentine's wakiwa kwa gari moja.

“Zuchu ni msanii wangu na sio mara ya kwanza kuja naye redcarpet.Nilikuja naye mara ya kwanza nikamtambulisha alikuwa mtoto. Amekuwa sasa ni msanii mkubwa. Kwa hivyo namleta tena, Mtoto kwa baba hakui,”alisema Diamond.

Ikumbukwe ni hivi majuzi, Zuchu alikuwa amedokeza kwamba siku ya wapendanao , Februari 14 atakuwa na mpenzi wake kwenye tamasha yake,kitu kilichokuwa kimesubiriwa kwa hamu na ghamu.

Vilevile, Diamond aligusia mambo na mahusiano yake, alieleza kuwa yupo kwenye mahusiano yanayofanya vizuri na hivi karibu ataweka wazi mahusiano yake na kuwaomba mashabiki kuendelea kusikiza kazi zake.