Shiti amsherehekea mwanawe na kusisitiza hajawahi kosa kumshughulikia

Muhtasari

• Mchekeshaji DJ Shiti alimsherehekea mwanawe siku ya Valentino na kusema kwamba anajivunia sana kuwa baba na kwamba hawajahi hata siku moja kukosa kumshughulikia

• Siku chache zilizopita, aliyekuwa mkewe Shiti na ambaye ni mzazi mweziwe,  aliibua madai kwamba mchekeshaji huyo hamshughulikii mwanao

DJ SHITI NA OMOSH WAKIIGIZA
DJ SHITI NA OMOSH WAKIIGIZA

Mchekeshaji DJ Shiti alimsherehekea mwanawe siku ya Valentino na kusema kwamba anajivunia sana kuwa baba na kwamba hawajahi hata siku moja kukosa kumshughulikia mwanawe katika mahitaji ya kimsingi tangu azaliwe.

Siku chache zilizopita, aliyekuwa mkewe Shiti na ambaye ni mzazi mweziwe, aliibua madai kwamba mchekeshaji huyo hamshughulikii mwanao na ametelekeza majukumu yake yote kama baba mzazi.

Shiti akizungumza katika mahojiano alisisitiza kwamba yeye hangependa kuzungumzia suala hilo kwani linakaa kifamilia Zaidi na hangetaka kulizungumzia bayana mbele ya kamera au kwenye simu ya wakuza maudhui wa mitandaoni.

Siku ya Valentino, kwa kile kilichoonekana kama kujibu madai ya mkewe, Shiti aliipakia picha ya binti yao kwenye instastories na kumsherehekea huku akimtata akue kwa haraka ili amuoneshe mchawi ni nani.

“Heri njema za siku ya Valentino Mariam Auma. Siku ukikua nitakwambia nani mchawi mamangu…Nakupenda sana mluhya wangu,” aliandika Shiti kwenye picha hiyo ya bintiye.

Vile vile, DJ Shiti alisisitiza kwamba yeye siku zote ni baba mwema na hajawahi kosa kumshughulikia binti yake kama inavyodaiwa na aliyekuwa mke wake.

“Ninachokijua mimi sijawahi kosa kukushughulikia hata siku moja tangu uzaliwe,” aliendeleza kuandika Shiti.