Mchekeshaji Eric Omondi atambulisha kipenzi chake hadharani siku ya wapendanao

Muhtasari

•Mchekeshaji  Eric Omondi  alionyesha Mpenzi  wake kwenye ukurasa wake instagram huku akimtakia siku njema ya wapendanao.

Eric Omondi
Eric Omondi
Image: INSTAGRAM// ERIC OMONDI

Mchekeshaji  Eric Omondi  alitambulisha mpenzi  wake siku ya Jumatatu kupitia ukurasa wake instagram huku akimtakia siku njema ya wapendanao.

Wanamitandao walichwa vinywa achama  kwani sio wengi waliotarajia  mcheshi huyo kupiga hatua kama ile.

Omondi alionekana pamoja na mwanadada anayetambulika kama Lyne wakiwa wamevaa mavazi mekundu.  

Kama ilivyokawaida siku ya wapendanao kupostiana na kuandikiana maneno yenye hisia za mapenzi, Mcheshi huyo hakusazwa nyuma ambapo alichukua nafsi hiyo kumwonyesha mwanadada huyo mahaba.

Ikumbukwe ni hivi majuzi Mcheshi huyo alindokeza kwamba alimpatia  Lyne gari lake na hana haraka ya kulichukua.

 Mcheshi huyo alikuwa miongoni mwa wanaume waliohudhuria  Men Conference siku ya Jumatatu  lakini alichukua fursa hiyo ya kipekee kuonyesha ulimwengu kuwa ana  kipenzi cha roho yake.

Wengi wanamjua Eric Omondi kama mchekeshaji mwenye vituko na sarakasi ambazo humsaidia kutengeneza kiki lakini  tokea hili ni kweli  mapenzi ni kikohozi hayafichika.