'Si rahisi kumpata Nyashinski' Juma Jux akiri

Muhtasari

•Alikiri  amekuwa akitembea nchini Kenya ili kuweza kufanikisha azimio lake la kushoot video ya wimbo wake na Nyashinski lakini imemchukua takribani mwaka mmoja kumpata.

Juma Jux
Juma Jux

Mwanamuziki wa Bongo Flava Juma Mussa Mkambala almaarufu Juma Jux ameeleza kuwa si kazi rahisi kumpata msanii wa humu nchini Nyashinski.

Akiwa kwenye mahojiano na kituo kimoja cha radio cha hapa nchini, Jux alikiri  kwamba amekuwa akitembea Kenya ili kuweza kufanikisha azimio lake la kushoot video ya wimbo wake na Nyashinski lakini imemchukua takribani mwaka mmoja kumpata.

Vilevile, alifichua kuwa mojawapo ya ndoto zake ilikuwa kufanya kazi na rapa huyo maarufu kote Afrika Mashariki.

Siku ya wapendanao Nyashinski alifanya show  ambayo ilihudhuriwa na watu wengi ajabu huku akiwashukuhuru mashabiki wake kwa kusimama naye kwa kipindi kirefu.

 “Ana kipaji na nilijua haikuwa rahisi kumpata, lakini nilitarajia kufanya naye kazi,” Juma Jux alisema.

Alieleza kuwa walianza mazungumzo na Nyashinski kupitia ukurusa wa Twitter ambapo alimpongeza kwa kibao alichokuwa  ametoa wakati huo  na  mazungumzo yao yaliendelea kuboreka hadi akamuomba Collabo.

Kulingana naye Collabo ilichukua mwaka moja kufanyiwa video kwani ilikuwa si kazi rahisi kumpata Nyashinki.

. “Alivutiwa na  wimbo wangu  na ndani ya siku mbili, alinitumia verse yake, lakini ilichukua mwaka kufanya video hiyo. Kila kitu kilikuwa kimewekwa tayari  lakini alikuwa hapatikani hata kwenye simu. Nilienda kumtafuta mara si moja lakini mwishowe nilifanikiwa kumpata” alisema Jux