Jihathari na wapenzi wanaojipenda katika mahusiano, Benjamin Zulu ashauri

Muhtasari

• Mshauri wa ndoa na kisaikolojia Benjamin Zulu amewaonya watu walioko kwenye mapenzi kujitahathari sana na wapenzi wanaojipenda.

• “Katika mahusiano kama hayo, si wewe tatizo, watu kama hao huwezi kuwarekebisha…jiokoe,” aliusia Zulu.

Benjamin Zulu
Image: Facebook

Mshauri wa ndoa na kisaikolojia Benjamin Zulu amewaonya watu walioko kwenye mapenzi kujitahathari sana na wapenzi wanaojipenda ambao aliwaelezea kuwa na tabia za kinazi, ‘narcissists’

Mshauri huyo mwenye utata akiandika kwenye ukurasa wake wa Facebook aliwataka wapenzi kuwa macho sana na watu kama hao kwani ukiwaegemea sana mwisho wa siku utakuwa unaumia kuvunjwa moyo.

Zulu ameelezea watu wenye tabia ka kihivyo kuwa wana tabia ya kufanya mambo yasiyostahili ili kujiridhisha na nafsi zao wenyewe, ambapo watakuwa wachepukaji wa kipigiwa mifano na walaghai wa pesa, mradi tu kuzitosheleza nafsi zao.

“Watu kama hao mara nyingi huwa hawatosheki na mambo au vitu vya kawaida kama vile ambavyo vinaridhisha mtu wa kawaida kama kuwa na mpenzi mmoja au hata kuwa katika mahusiano yenye furaha na amani,” aliandika mwanasaikolojia huyo.

Mshauri huyo wa ndoa alizidi kuelezea kwamba watu wa namna hiyo watamfanya mtu kutia jitihada na bidi katika kazi zao ili kufanya mahusiano kuwa ya amani, lakini nyuma ya pazia wanapalia kukutamausha na kukuvunja moyo.

“Katika mahusiano kama hayo, si wewe tatizo, watu kama hao huwezi kuwarekebisha…jiokoe,” aliusia Zulu.