Niko tayari kwa lolote mwanangu aishi maisha mazuri-Amber Lulu kwa wakosoaji

Muhtasari
  • Aidha msanii huyo amesema kwamba yuko tayari kwa lolote ili mwanawe aishi maisha mazuri, kwani hakumzaa ili aanze kuomba msaada kutoka kwa wanamitandao
Amber-Lulu-eating-food(1)
Amber-Lulu-eating-food(1)

Amberlulu ni msanii wa muziki wa Tanzania, mwigizaji na mshawishi,  Anajivunia wafuasi wengi milioni 3.7 kwenye Instagram.

Hata hivyo, ukipitia akaunti yake ya instagram, mwanamuziki huyo mwenye uzoefu amewajibu wale wanaomdharau kupitia stori yake ya insta kwa kushirikishwa kwenye video ya msanii wa muziki wa Konde Gang Worlwide, Anjella.

Anakiri kwamba baada ya kupitia maoni ya watumiaji wengi wa kijamii kwenye akaunti yake ya instagram, wengi wamemlaumu kwa hili.

Aidha msanii huyo amesema kwamba yuko tayari kwa lolote ili mwanawe aishi maisha mazuri, kwani hakumzaa ili aanze kuomba msaada kutoka kwa wanamitandao.

"Unajua nimeona comment zenu nyingi kuhusu mimi, kufanya video ya Angela nafanya kila kitu ambacho kitaniingizia pesa halai kumbukeni mimi ni mama nae lea mtoto angu mwenyewe kwa hivyo niko tayari kwa lolote ili mwanangu aishi maisha mazuri na bora zaidi kuliko mimi

Kwa hivyo nimelipwa, nikatae pesa kwa sababu nashusha brand huku mwanangu analia njaa kama wewe ni mwanamke na single mother unanielewa au mnataka mje mnichangie insta au niwalilie humu insta kwani nimewazalia insta.

Nilizaa kwa mapenzi yangu mwenyewe mambo ya kujiliza liza sio vitu vyangu ile ni kazi na nimepata pesa ama mlitaka nikauze mwili wangu."