Kwa nini msanii Size 8 alifunganya virago na kuiacha ndoa yake

Muhtasari
  • Mnamo 2018, alitoka nje ya ndoa yake na kukodisha nyumba yake mwenyewe

Mwimbaji wa nyimbo za Injili Size 8 anasema ndoa yake na DJ Mo haikuwa rahisi na wakati fulani, alikusanya virago na kuondoka.

Akizungumza kwenye mahojiano na Kiss FM, mama huyo wa watoto wawili alisema mwaka 2016 alimfungia mumewe nje na kutupa vitu vyake nje baada ya kutofautiana.

Mnamo 2018, alitoka nje ya ndoa yake na kukodisha nyumba yake mwenyewe.

"Ndiyo nimehama lakini si hivi majuzi ni 2018 ndio nilitoka nje? Yeah I did! Nikatoka nika pack na nika get hao yangu. Unajua ninachokipenda mimi na mume wangu tuko wakweli kuhusu matembezi yetu ya ndoa.Ndoa ni safari nzuri lakini ina misukosuko yake na mimi kabla sijapevuka katika mambo mengi niliwahi kuyatenda sana." Alisema.

Kuongeza, hata kuna siku ilikuwa 2016 nilimfungia Mo nje ya nyumba. Nilimfungia nje akakuja akakuta vitu vyake na mlango nimefunga

Alisema kwamba katika siku zake za ndoa ya mapema, alikuwa anakasirika kupita kiasi kwa masuala madogo.

"Nimesumbua sana, nimepaki na kuondoka na nimezidi sana. Nimefanya yote hayo na namshukuru Mungu kwa sababu sasa hivi nashughulikia mambo kwa ukomavu tofauti kabisa," alisema.

Aliongeza kuwa yeye huzungumza kuhusu matukio yake ili kuwatia moyo wanandoa wengine.

"Ninachopenda mimi na mume wangu, ni wakweli katika matembezi yetu ya ndoa, ndoa ni safari nzuri lakini ina misukosuko yake."

Aliongeza, "Ninapenda kuwa mwaminifu kwenye ndoa kwa sababu unapokuwa mwaminifu, unawatia moyo watu wengine, unapochora picha ya ukamilifu, unawafanya watu wengine wajisikie wako kuzimu...naweza kusema kweli nimekomaa na Sipaki na kufuata kila mabishano."