Mwanadada atangaza kuambukiza watu 134 na virusi vya Ukimwi

Muhtasari

• Mwanmke mmoja kutoka nchini Nigeria amewashangaza wengi baada ya kuweka wazi kwamba amewaambukiza watu 134 na virusi vya Ukimwi tangu mwaka wa 2016.

• Alisema kati ya hao, 115 ni wanaume huku 19 wakiwa ni vwanawake.

Afro Sophia
Afro Sophia
Image: Twitter

Mwanamke mmoja nchini Nigeria ameaacha wengi vinywa wazi baada ya kudai kwamba amewaambukiza watu 134 na virusi vya ukimwi.

Afro Sophia, kama anavyojitambulisha Twitter amesema kuwa ameabukiza takriban wanaume 115 na wanawake 19 tangu mwaka wa 2016 alipopatikana na virusi hivyo. Alifuchua  maneno haya yenye ukakasi mkubwa alipokuwa akijibu ‘tweet’ ya mwanadada mwingine, Nelly Nesh19 ambaye amekuwa akiishi na virusi hivyo.

Katika ujumbe wake wa kuhamasisha watu wanaoishi na virusi hivyo, Nesh19 aliandika kuwa aliambukizwa virusi vya ukimwi akiwa na miaka 21 na mpaka sasa ana miaka 24 na anaishi vizuri tu.

Hapo ndipo Sophia alivunja ukimya na kusema kwamba tangu agundue ana virusi miaka sita iliyopita amekuwa katika msururu wa kuhakikisha anawaambukiza watu wengi kadri ya uwezo wake, bila kubagua jinsia wala umri.

“Niliambukizwa virusi vya ukimwi nikiwa na umri wa miaka 21, sasa hivi nina miaka 24 na niko sawa na virusi hivyo,” aliandika Nelly.

Niliambukizwa na rafiki wa karibu wa kakangu mwaka 2016 nikiwa na umri wa miaka 18 tu. Alikuwa mvulana wa kwanza na pekee niliyefanya naye mapenzi hadi nilipofikisha umri wa miaka 20. Tangu Desemba 2017 nilipimwa na kupata niko chanya, niliweka dhamira yangu kuwapa wengine kile ambacho niliambukizwa, bila kondomu. Karibu wavulana 115 na wasichana 19 sasa na bado naendelea kuhesabu,” aliandika Sophia.

Maneno haya yake yasiyokuwa na kujutia yamepokewa kwa ukosoaji mkubwa huku wengi wakimshtumu kwa kuwasambazia watu wasio na hatia, kisa na maana aliambukizwa na mwanaume wa pekee katika maisha yake.