"Nina ukimwi lakini sijawahi ambukiza mtu" - Doreen Moracha

Muhtasari

• Shujaa aliyeshinda vita dhidi ya unyanyapaa wa watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi Doreen Moraa Moracha anasema mahusiano yake yote yamekuwa na watu wenye hali hasi lakini hajawahi ambukiza hata mmoja.

Doreen Moraa Moracha
Image: INSTAGRAM

Shujaa aliyeshinda vita dhidi ya unyanyapaa wa watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi Doreen Moraa Moracha amefunguka na kusema kwamba hata ingawa yeye ni muathirika wa virusi hivyo, lakini mahusiano yake yote amekuwa na watu wasiokuwa na virusi hivyo na hajawahi muambukiza hata mmoja.

Akiandika kwenye ukurasa wake wa Instagram, Moraa amesema kwamba hajawahi ambukiza mtu hata mmija virusi vya Ukimwi na kusisitiza jukumu lake kuu ili kumaliza virusi hivyo ji kumeza tembe za ARV kama alivyoratibiwa na madaktari wake.

“Sijawahi kuwa katika mahusiano ya kimapenzi na mtu mwenye hali chanya ya virusi vya ukimwi kama mimi, lakini pia sijawahi muambukiza mtu yeyote virusi hivi kwa sababu najua jukumu langu katika kuvimaliza ni kumeza ARV ili kumlinda mpenzi wangu asipate virusi hivi kutoka kwangu,” aliandika Doreen kwenye Instagram.

Jambo hili liliwashangaza wengi ambao walionekana kutoamini kwamba mtu mwenye virusi anaweza kuwa katika mahusiano na mtu vasiye na virusi hivyo na bado asimuambukize, Doreen alifafanua Zaidi kwamba hili linawezekana kwa kusema kwamba njia pekee ni kumeza vidonge vya ARV ili kupunguza makali ya virusi hivyo mwilini na hivyo kutosambaa kwa mtu aliye na hali hasi.

Moracha amekuwa balozi wa kuhubiri dhidi ya unyanyapaa kwa wale wanaoishi na virusi vya ukimwi na mwaka wa 2020 alishinda tuzo ya Stigma Warrior katika tamasha la International Stigma Conference kwa kujitokeza na kupinga kunyanyapaliwa kwa wahathirika wa virusi hivyo.

Moracha alizaliwa na virusi hivyo na ameishi navyo kwa Zaidi ya miaka 29 sasa. Ama kweli ni shujaa!