Bintiye Akothee, Rue Baby azungumza kuhusu madai ya kuchumbiana na mzungu

Muhtasari

• Rue Baby amewaomba wanamitandao waache uvumi huku akisisitiza kuwa hakusema ni mpenzi wake.

• Kando na mzungu huyo asiyetambulishwa, Rue Baby amewahi kudaiwa kuwa kwenye mahusiano na mchekeshaji MCA Tricky.

Binti wa pili wa Akothee, Agrrey Dion Okello almaarufu Rue Baby alilazimika kueleza video yake akijivinjari na mzungu baharini ambayo alipakia Instagram baada ya wanamitandao kutaka kujua kuhusu uhusiano wake naye. 

Kwenye ukurasa wake wa Instagram, Rue Baby alipakia video iliyoonyesha miguu yake na ya mwanaume mzungu kisha kuiambatanisha na emoji za mapenzi.

Wanamitandao wengi walijijazia kwamba mwanamitindo huyo yuko kwenye likizo na mzungu huyo ambaye walishuku kuwa ni mpenzi  wake.

Akizungumzia madai ya mwanaume huyo kuwa mpenzi wake, Rue Baby aliwaomba wanamitandao waache uvumi huku akisisitiza kuwa hakusema ni mpenzi wake.

"Wacheni pupa. Sijasema  ni wangu. Labda miguu ni ya jirani jameni  pthooo," Rue Baby alisema

Kando na mzungu huyo asiyetambulishwa, Rue Baby amewahi kudaiwa kuwa kwenye mahusiano na mchekeshaji MCA Tricky.