Mafuta ya Arimis miongoni mwa bidhaa pendwa na wanawake Kenya - IPSOS, BSD Group

Muhtasari

• Katika orodha hiyo, nafasi za mwanzo nne zilichukuliwa na Safaricom,Mpesa, Airtel, Equity na ya tano bora ikashangaza wengi ambapo Arimis ilijinafasi hapo kama bidhaa inayopendwa zaidi nchini.

Mafuta ya kujipaka ya Arimis
Mafuta ya kujipaka ya Arimis
Image: Maggy Shawn

Kampuni za utafiti za IPSOS na ile ya BSD Alhamis walitoa orodha ya bidhaa ambazo zinapendwa zaidi na Wakenya wanawake.

Katika orodha hiyo, bidhaa kama mtambo wa kutuma pesa wa M-Pesa na mafuta ya kujipata na kukamua ya Arimis ni baadhi ya bidhaa pendwa zaidi miongoni mwa Wakenya wanawake.

Katika orodha hiyo, nafasi za mwanzo nne zilichukuliwa na Safaricom,Mpesa, Airtel, Equity na ya tano bora ikashangaza wengi ambapo Arimis ilijinafasi hapo kama bidhaa inayopendwa zaidi nchini.

Mkurugenzi mkuu wa kundi la BSD, Eva Muraya alisema kwamba 80% ya matumizi ya bidhaa hizi hufanywa na wanawake nchini.

Sampuli ya utafiti ilitolewa kutoka Pwani, Kaskazini Mashariki, Mashariki, Kati, Bonde la Ufa, Magharibi, Nyanza na Nairobi na ilihusisha wanawake kutoka rika mbalimbali na hali ya kijamii na kiuchumi.

Utafiti kama huu ambao ulifanywa mwaka jana ulionesha mafuta ya Arimis yakiwa yameshikilia nambari 7 katika orodha ya bidhaa 100 pendwa zaidi miongoni mwa wanawake nchini Kenya.

Kwa upande mwingine, kupoteza familia, kuugua sana, kushindwa kufikia malengo ya maisha, kutokuwa na uwezo wa kuweka chakula mezani na ukosefu wa ajira ndio hofu kuu ya wanawake katika mpangilio huo, kulingana na uchunguzi.