Zari afunguka jinsi alivyojaribu kuokoa ndoa yake na Diamond Platnumz

Muhtasari

•Zari alisema kuwa angelalamikia tabia zake mbaya kila wakati, lakini Diamond mwenyewe hakushughulika.

•Zari alikatiza mahusiano yao baada ya Diamond  kumpa ujauzito Hamisa Mobetto na hiyo ilikuwa thibitisho kuwa hakuwa mwaminifu.

Zari Hassan na Diamond Platnumz walipokuwa kwenye mahusiano
Zari Hassan na Diamond Platnumz walipokuwa kwenye mahusiano
Image: HISANI

Zari alisema anafahamu baba ya watoto wake wawili Diamond alikuwa anatoka nje ya ndoa lakini aliamua kuyafumbia macho.

"Hata nyakati ambazo nilijua umekosea, ningenyamaza tu kwa ajili ya amani, tufurahie, tuyaache yaende, tusonge mbele, tuendelee na kuweka familia..."

Mama huyo wa watoto watano aliongeza kuwa angelalamikia tabia zake mbaya kila wakati, lakini Diamond mwenyewe hakushughulika.

"Ningekubali kupigwa risasi kwa ajili yako, lakini kila nilipokufanyia hivyo, ulifanya kinyume, mimi na watoto wako tulikuwa tukivamiwa, sikuwa na mahali pa kujificha," alisema.

Zari alikatiza mahusiano yao baada ya Diamond  kumpa ujauzito Hamisa Mobetto na hiyo ilikuwa thibitisho kuwa hakuwa mwaminifu.

"Watu hao wakioanza kutoa risiti za tabia zako, ulichofanya, na risiti ziko mbele ya macho yetu, mimi hujiondoa na kusema ndio, alifanya hivyo."

Kwa sasa Zari anatoka kimapenzi na bwenyenye wa Uganda anayetambulika kwa jina la GK Choppa.

"Nilisonga mbele, nina furaha nilipo na nina uhakika Diamond anafurahi pale alipo, lakini binafsi, ni kitu ambacho kinaendelea kurudi. Nilikuwa na kitu kizuri na kiliharibika."

(UTAFSIRI: SAMUEL MAINA)