"Hatushiriki tendo la ndoa," Zari afafanua kuhusu uhusiano wake na Diamond Platnumz

Muhtasari

•Mama huyo wa watoto watano alieleza kuwa Diamond hutembea kwake mara kwa mara kwa ajili ya kuona watoto wao wawili, Tiffah Dangote na Prince Nillan.

• Mara nyingi Diamond ameshtumiwa kwa kuwapenda watoto wake na Zari zaidi ya wengine wawili ambao alipata na Hamisa Mobetto na Tanasha Donna.

Zari Hassan na Diamond Platnumz
Zari Hassan na Diamond Platnumz
Image: INSTAGRAM// TIFFAH DANGOTE

Mwanasoshalaiti na mfanyabiashara mashuhuri kutoka Uganda Zari Hassan ameweka mambo bayana kuhusu uhusiano wake wa sasa na aliyekuwa mpenzi wake Diamond Platnumz.

Akizungumza katika shoo ya 'Young, Famous and African' ambayo ameshirikishwa pamoja na baadhi ya wasanii wengine wakubwa wa Afrika, Zari aliweka wazi kuwa kwa sasa hakuna uhusiano wowote wa kimapenzi kati yake na Diamond.

Mama huyo wa watoto watano alieleza kuwa Diamond hutembea kwake mara kwa mara kwa ajili ya kuona watoto wao wawili, Tiffah Dangote na Prince Nillan.

"Mimi na Diamond hatujarudiana. Huwa anakuja kutembea kisha anaenda. Hatuko pamoja, hatushiriki tendo la ndoa, hata hatulali pamoja ama kugusana," Zari alisema.

Mwanasoshalaiti huyo ambaye kwa sasa anashughulikia biashara zake Afrika Kusini alijigamba kwamba hahitaji mwanaume ili kufanikiwa maishani.

"Mimi ni bilionarre, sihitaji mwanaume," Alisema.

Zari pia alidai kuwa hakuna uhasama wowote kati yake na Diamond huku akieleza kuwa wao ni marafiki wakubwa.

Wengi wamekuwa wakitilia shaka uhusiano wa wawili hao kutokana na jinsi huwa wanaonekana pamoja mara kwa mara. Mara nyingi Diamond ameshtumiwa kwa kuwapenda watoto wake na Zari zaidi ya wengine wawili ambao alipata na Hamisa Mobetto na Tanasha Donna.