Alikuwa anasema mimi ni dem wake kabla kunitongoza - mpenzi wa Simple Boy

Muhtasari

• Alikuwa anaweka rumours kwamba mimi ni dem wake ilhali am not. 

• Nilikuwa napigana na watu kumbe yeye ndiye alikuwa anawaambia mimi ni mpenzi wake bila mimi kujua - Pritty Vishy

Pritty Vishy, Stivo Simple Boy
Pritty Vishy, Stivo Simple Boy
Image: INSTAGRAM

Mwanablogu na ambaye ni mpenzi wa msanii Stivo Simple Boy, Pritty Vishy amezungumza jinsi mapenzi yao yalivyoanza na kukolea na msanii huyo kutoka Kibera ambaye inahusunisha sana jinsi amekuwa akichambwa mitandaoni kutokana na muonekano wake.

Pritty Vishy katika video yake kwenye mtandao wa YouTube katika kile alisema ni kumtambulisha Simple Boy kwa mashabiki wake, alifichua kwamba msanii huyo alikuwa akidanganya watu kwamba yeye ni mpenzi wake hata kabla ya kumtongoza.

Vishy anasema jambo hilo lilimfitinisha na watu wengi mpaka kupelekea kupigana na wale waliokuwa wanamuita mpenzi wa Stivo hali ya kuwa yeye anajua ni urafiki tu wa kawaida.

“Nishawahi pigana cos alikuwa anaweka rumours kwamba mimi ni dem wake ilhali am not, so ikabidi nimepigana wewe, unaniitaje dem wa Stivo Simple Boy msee na he is just my friend, kumbe yeye ndiye alikuwa anaenda anawaambia hivo,” Pritty Vishy anasema.

Mwanadada huyo ambaye wengi wamemjua kwa sapoti yake kubwa kwa kazi za mpenzi wake Stivo Simple Boy alisema kwamba hayo yalikuwa ya kitambo na sasa hivi wanapendana.

Pia alisema hivi karibuni wataanza kupiga kazi ya kukuza maudhui kwenye mtandao wa YouTube pamoja. Wapenzi hao wawili wamekuwa wakipendana na kuachana kwa mikupuo.