Je, Samidoh anamkosa Karen Nyamu, anataka warudiane?

Muhtasari

• Samidoh alipakia video ya ngoma ya Salim Junior yenye maudhui ya kumtaka Njeri kurudi nyumbani, wanamitandao wakakisia huenda anataka kurudiana na Karen Nyamu ambaye jina lake la kati ni Njeri.

Karen Nyamu, Samidoh
Karen Nyamu, Samidoh
Image: INSTAGRAM

Siku kadhaa baada ya uvumi kusambaa kwamba hatimaye mwanamuziki na polisi Samidoh wameachana na mchepuko wake ambaye ni mwanasiasa Karen Nyamu, pia palizuka taarifa nyingine kwamba staa huyo wa Mugithi ametengana na mke wake Edday, wanawake wote wakisemekana kuwa na ujauzito wake.

Samidoh sasa kwa siku za hivi karibuni ameonekana kuwa roho juu sana akionesha dalili zote amekosa mapenzi sana.

Juzi kati msanii huyo amepakia video fulani kwenye ukurasa wake wa TikToq akiimba ngoma ya msanii mwenzake wa Mugithi, Salim Junior ambapo ujumbe na maudhui ya ngoma hiyo ni kumtaka Njeri kurudi nyumbani.

Ikumbukwe pia Njeri ni jina la pili la Karen Nyamu na pia ndilo jina amempatia binti wake. Wengi walioiona video hiyo ya Samidoh akiimba nyuma ya sauti ya Salim Junior kumtaka Njeri kurudi nyumbanii walihisi kwamba Samidoh anajaribu kutuma ujumbe wa kutaka maridhiano na Njeri, ambaye ni Karen Nyamu.

Samidoh walipapurana na Nyamu kupitia kila mmoja wao kufanya video yenye maudhui fiche yanayomlenga mwingine huku Samidoh akifanya video ya kutuma ujumbe kwamba hatajukumika kwa malezi ya mtoto-kijajo na Nyamu akajibu kwa kufanya video yenye ujumbe wa kutomshrutisha mwanaume kukubali majukumu ya uzazi.