Harmonize: Mungu rudisha familia yangu, samahani binti yangu kwa mazingira magumu

Muhtasari

Harmonize - Mungu irudishe familia yangu tafadhali. Samahani sana binti yangu. Bado nakumbuka nyakati zile tukiwa pamoja kama familia

Harmonize na aliyekuwa mpenzi wake Sarah Michelotti
Harmonize na aliyekuwa mpenzi wake Sarah Michelotti
Image: THE STAR

Je, msanii Harmonize ameingia mkondo wa kusongwa na mawazo kutokana na kutengana na familia yake kama staa wa Marekani wa hiphop Kanye West?

Maswali kama haya yametanda vichwqani mwa watu wengi ambao wanamfuatilia msanii huyo kwa ukaribu na pia kuyafuatilia matukio katika Sakata la kutalikiana baina ya Kanye West na mpenzi wake wa miaka 12, Kim Kardashian.

Harmonize wikendi iliyopita alionekana akituma ujumbe changamano kwa mpenzi wake kupitia instastories zake ambapo anasononeka pakubwa mpaka kumtaka Mungu airudishe familia yake, kwa kutumia maneno yale yale ambayo pia Kanye West aliwahi yatumia wakati mmoja akiomba Mungu kuirudisha familia yake.

“Mungu irudishe familia yangu tafadhali,” aliandika Harmonize kwenye instastories zake.

Kwa mara ya kwanza hakuna aliyejua msanii huyu alikuwa anazungumzia familia ani kutokana na kwamba amekuwa katika mahusiano mara mbili kabla ya mahusiano ya sasa.

Baadaye ilionekana kwamba Harmonize anaikosa sana familia yake na mchumba wake Muitaliano Sarah Michelotti ambaye walifanikiwa naye mtoto mmoja wa kike, Zulekha Nasra.

Katika kipande kingine Harmonize aliachilia ujumbe mzito kwa mwanawe Zulekha huku akimtaka radhi kwamba ikatokea amekufa leo bila kumwomba msamaha kwa kumweka katika mazingira magumu basi atakuwa mjinga wa kupigiwa mfano.

“Samahani sana binti yangu. Nitakuwa mtu mjinga sana kama nitakufa leo bila kusema samahani kwa kukuweka katika mazingira magumu, haswa kutokana na umri wako ulivyo mdogo. Ninahisi vibaya sana haswa nikiwa baba wa mabinti na singependa kuingia ndani sana kwa sababu inauma. Ila zidi kujua tu kwamba nakupenda sana, endelea kumfanya mamako kujivunia. Bado nakumbuka nyakati zile tukiwa pamoja kama familia, najivunia sana kwa mtu ambaye unakua kukuwa. Mungu akulinde, ila samahani sana,” aliandika Harmonize