Utafiti: Wanawake wengi hawafiki kilele kiasi cha kuachilia michirizi wanapojamiana

Muhtasari

• Utafiti ambao umefanywa na wanasayansi wa afya ya mwili na mahusiano ya kingono unaonesha kwamba asilimia 10 tu ya wanawake wanaoshiriki ngono hupata mchemko wa kutokwa na unyevunyevu mkali wakati wa tendo la ndoa.

Maktaba
Maktaba

Utafiti ambao umefanywa na wanasayansi wa afya ya mwili na mahusiano ya kimapenzi unaonesha kwamba ni asilimia 10 tu ya wanawake wanaoshiriki tendo la ndoa  ambao kuafikia kilele cha ngono kiasi cha kuachilia michirizi ya uke (squarting) .

Kati ya asilimia 50 hadi 80 ya wanawake hawajawahi toa michirizi ya uke wakati wa tendo la ndoa na aghalabu hujifanya tu kwa kuigiza kwamba wamepata mhemko huo wa ngono ili kuliwaza nafsi za wapenzi wao wa kiume.

Kulingana na Wairimu Njeri, 25, katika mahojiano ya kipekee na gazeti la The Star, katika maisha yake huwa anasikia tu kuhusu michirizi ya kingono ingawa yeye mwenyewe hajawahi kufikia kilele hicho.

“Huwa nasikia kwamba kupata mhemko wa kingono ni jambo linaloweza kutokea lakini kwangu mimi halijawahi tokea. Inafikia mahali ninafikiria mimi na mpenzi wangu huenda tunafuata mkondo mbaya katika kufanya tendo la ndoa mpaka sipati michirizi au pengine mimi ndio tatizo,” alisikitika Njeri.

Kulingana na mtaalam wa afya ya uzazi Ann Kihara watu wengi wanajiweka katika shinikizo la kutaka kupata mhemko wa kingono, alisema watu wengi wanaposikia kuhusu kuchemka huko moja kwa moja taswira inayojengeka mawazoni mwao ni bomba la maji linalotupa maji kwa kunyunyiza, na hapo ndipo wanapotoka kifikira.

“Kupatwa na hali hiyo ya kuchemka na kuachia unyevunyevu ni kweli na ni aina mojawapo ya kutoa nii. Lakini mara nyingi hutofautiana kutoka kwa mtu hadi mwingine. Baadhi ya wanawake wanaweza kutetema, kunyunyiza, kububujikwa au hata kutokwa na mchemko huo kwa nguvu. Ukweli ni kwamba, yote inategemea mwili wa kila mtu na anatomia yake,” alielezea Kihara.

Mtaalamu huyo aliwaondolea wasiwasi wanawake wanaojishuku kwamba huenda wanafanya tendo la ndoa vibaya na ndio sababu ya kutofikia kilele cha kupata michirizihiyo. Alisema kwamba miili ya wanawake inatofautiana kwani kuna wengine wanafika kilele na kupata mchemko huo wa kutokwa na chemchemi huku kuna wengine wanafikia kilele na kuhisi kuridhika tu bila mchemko na pia wengine waliobahatika sana hupatwa na yote mawili.

"Ninawaambia wateja wangu kwamba ngono ni kama safari, furahiya mchakato huo na uache kulenga sana katika kilele. Kubali majibu ya mwili wako, ikiwa itatokea basi ni vizuri na kama la haijatokea pia ni sawa. Kila mtu ni wa kipekee,” alimaliza Kihara.