Utafiti: Vidonge vya kupanga uzazi kwa wanaume vina ufanisi 99%

Muhtasari

• Utafiti unaonesha vidonge vya kupanga uzazi kwa wanaume vina ufanisi wa hadi 99%.

Vidonge
Vidonge
Image: THE STAR

Baada ya kuzama na kulivalia njugqa suala la kutafuta mbinu mbadala ya upangaji uzazi wa upande wa wanaume, wanasayansi hatimaye wameibuka na habari mpya ambapo wamedhibitisha kwamba wametengeneza tembe za kutumiwa na wanaume ili kupanga uzazi.

Wanasayansi hao wanasema walifanya vipimo vya maabara kwa panya na vipimo hivyo vilipata kwamba tembe hizo zina ufanisi wa hadi ailimia 99 kufanya kazi vizuri katika upangaji uzazi bila kufeli.

Hii inakuja kama habari mpya kwa wanaume ambao sasa watakuwa na njia mbadala nyingi tu za kuchagua kupanga uzazi baada ya muda mrefu kulazimika kuchagua baina ya mbinu chache zikiwemo kuchukua likizo ya ngono, matumizi ya kondomu za kiume na kufanyiwa upasuaji wa vasektomia, ambapo aghalabu huwa na gharama ya juu kando na kupoteza kabisa uwezo wa mwanaume kupeana mimba.

Utafiti huo ambao uliwasilishwa katika mkutano wa Jumuiya ya Kemikali ya Marekani umeeleza kwa kina kwamba katika panya, kidonge kilikuwa na ufanisi katika kuzuia mimba na hakikuleta madhara yanayoonekana.