"Umenikosea na umenikwaza" Kajala amkemea mwanahabari aliyeghushi meseji zake na shoga wake

Muhtasari

•Mpenzi huyo wa zamani wa Harmonize amesema amekerwa sana na kitendo cha mtangazaji huyo na kumwagiza amkome.

•Screenshot hizo za meseji zinadaiwa kuwa mazungumzo ya Kajala na rafiki yake kumhusu mwanamuziki Harmonize.

Image: INSTAGRAM// FRIDAH KAJALA

Mwigizaji Fridah Kajala Masanja ameeleza ghadhabu yake kwa mtangazaji wa Bongo, Soud Victor Kadio kufuatia kile anachosema alighushi mazungumzo yake na rafiki wake wa karibu.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Kajala amesema amekerwa sana na kitendo cha mtangazaji huyo na kumwagiza amkome.

Mpenzi huyo wa zamani wa Harmonize ameweka wazi kwamba meseji hizo zinazoenezwa  kwenye mitandao ya kijamii hazina ukweli wowote.

"Usione nakaa Kimya ukazani mimi mjinga. Lakini ilipofikia wewe kutunga meseji kuonyesha jamii mimi nachat na mtu umenikosea sana na umenikwaza. Kama huna umbea wa kuandika siukae kimya kwani lazima uandike vitu vya uongo! Daah inasikitisha sana," Kajala amemwambia Victor.

Screenshot hizo za meseji zinadaiwa kuwa mazungumzo ya Kajala na rafiki yake kumhusu mwanamuziki Harmonize.

Katika meseji hizo, anayedaiwa kuwa shoga wa Kajala anaonekana akimhoji kuhusu sababu zake kutomkubali tena Harmonize licha ya juhudi zote alizotia kuomba msamaha.

Kajala amesisitiza kwamba meseji hizo ni za uwongo huku akidai mwanahabari huyo ametafuta umakini wake tu.