Pritty Vishy apingana na ex wake Stivo Simple Boy kuhusu suala la ngono kabla ya ndoa

Muhtasari

•Vishy amesema kuwa wapenzi wanafaa kufurahia tendo la ndoa hata kabla ya kufunga pingu za maisha.

•Stivo alifichua kuwa yeye bado ni bikra na kwa kuwa hataki kukiuka agizo la Biblia linalosema watu hawapaswi kushiriki ngono kabla ya ndoa.

Stivo Simple Boy na aliyekuwa mpenzi wake Pritty Vishy
Stivo Simple Boy na aliyekuwa mpenzi wake Pritty Vishy
Image: SCREENGRAB// MUNGAI EVE

Purity Vishenwa almaarufu Pritty Vishy amepingana na maoni ya aliyekuwa mpenzi wake Stivo Simple Boy kuhusu suala la watu kushiriki mchezo wa kitandani kabla ya ndoa. 

Vishy amesema kuwa wapenzi wanafaa kufurahia tendo la ndoa hata kabla ya kufunga pingu za maisha.

"Watu wasingoje. Hata ukienda kunua gari, lazima ujaribu ingini kama inafanya kazi," Vishy alisema katika mahojiano na SPM Buzz.

Hisia za Vishy kuhusu suala hilo zinapingana na zile za Stivo Simple Boy ambaye hivi majuzi alisema watu wanafaa kufunga ndoa kabla ya kushiriki mapenzi.

Stivo alifichua kuwa yeye bado ni bikra na kwa kuwa hataki kukiuka agizo la Biblia linalosema watu hawapaswi kushiriki ngono kabla ya ndoa.

"Mapenzi yanafaa kufanywa kama mtu ameoa ama ameolewa. Sio mambo ya kucheza cheza hapa na pale alafu msichana akishapata mimba  jamaa anatoroka. Hiyo haifai. Sijawahi kufanya mapenzi kwa kuwa bado sijaoa," Stivo alisema katika mahojiano na Eve Mungai.

Mwanamuziki huyo kutoka Kibra alidokeza kuwa mahusiano yake na Vishy yalifika kikomo baada ya kipusa huyo kusisitiza washiriki mapenzi, jambo ambalo hakukubaliana nalo kwa kuwa hawakuwa kwenye ndoa rasmi.

Alisema kuwa msimamo wake wa kukataa kushiriki mapenzi haukumfurahisha Vishy na ndiposa akaamua kumtema.

"Yeye hakutaka  kusikia. Alisema Simple Boy ameokoka sana ni heri aende kwa mwingine. Nilikataa," Alisema.

Vishy ameweka wazi kuwa sasa yupo single ila bado hayupo tayari kujaribu mahusiano mengine kwa sasa.

"Natafuta mchumba. Lakini wasianza kunitafuta saa hii. Wacheni kwanza nitafute pesa ata mimi," Alisema.

Vishy na Stivo walithibitisha kutengana kwao takriban miezi miwili iliyopita. Wakati huo Vishy alimshtumu mpenzi huyo wake kwa kumcheza na mwanadada mwingine.