Stivo alikuwa anatoka nje nikitaka kubadilisha nguo, hajui mwili wangu unavyokaa- Pritty Vishy

Muhtasari

•Vishy alisema mahusiano yao ya muda mrefu hayakuwahi kuhusisha shughuli yoyote ya kimapenzi.

•Vishy alidai kuwa Simple Boy hakuwahi kutaka kuona uchi wake na vilevile hakutaka wake naye uonekane kila walipokuwa pamoja.  

Image: INSTAGRAM// PRITTY VISHY

Pritty Vishy amefichua kuwa hakuwahi kuwa na uhusiano wowote wa kimapenzi na aliyekuwa mpenzi wake Stivo Simple Boy katika kipindi cha mahusiano yao.

Akiwa kwenye mahojiano na Eve Mungai, Vishy alisema mahusiano yao ya muda mrefu hayakuwahi kuhusisha shughuli yoyote ya kimapenzi.

Vishy aliweka wazi kuwa kamwe hajawahi kushiriki tendo la ndoa na msanii huyo kutoka Kibera wala kukumbatiana au kubusu.

"Hatujawahi ata kukumbatiana ama kubusu. Lakini alivyosema kuwa nilitaka tendo la ndoa ni uongo. Lakini hatujawahi kufanya chochote. Ata naweza kuapa kutumia Bibilia. Tulikuwa wapenzi.Hata alikuwa amenitambulisha kwa familia lakini hawakujua kuwa hatukuwa tunashirikitendo la ndoa. Sijui ilikuwa mahusiano ya aina gani," Vishy alisema.

Kipusa huyo pia alifichua kuwa hakuna yeyote ambaye aliwahi kuona uchi wa mwenzake kati yake na mpenziwe huyo wa zamani.

Alidai kuwa Simple Boy hakuwahi kutaka kuona uchi wake na vilevile hakutaka wake naye uonekane kila walipokuwa pamoja.  

"Ata hawezi kueleza mwili wangu unakaa aje. Kuna wakati nilikuwa naenda kwa Stivo, nikitaka kubadilisha nguo anaenda nje ama kama ako kwa kitanda anajificha na blanketi. Akitaka kubadilisha mbele yangu  alikuwa anavaa haraka haraka. Hatuwezi kueleza  jinsi mwili wa mwingine unavyokaa kwa sababu hatukuwahi kuonana," Alisema.

Vishy amefichua kuwa hakuwahi kuwa mwaminifu kwa mpenzi huyo wake wa zamani. Amedai kuwa hakuwahi kuvutiwa na mwanamuziki huyo.

Katika mahojiano ya hapo awali Simple Boy alikiri kuwa hajawahi kushiriki tendo la ndoa maishani mwake.

Alisema kuwa yeye ni muumini wa kweli na hayupo tayari kukiuka agizo la Bibilia linatahadharisha watu wasishirike ngono kabla ya ndoa.

"Mapenzi yanafaa kufanywa kama mtu ameoa ama ameolewa. Sio mambo ya kucheza cheza hapa na pale alafu msichana akishapata mimba  jamaa anatoroka. Hiyo haifai. Sijawahi kufanya mapenzi kwa kuwa bado sijaoa," Stivo alisema.

Mwanamuziki huyo pia alisisitiza kuwa kwa sasa  hana uhusiano wowote wa kimapenzi na Pritty Vishy ila wanashirikiana kikazi.