Ushauri wa Vera Sidika kwa wasichana wanaowachumbia wababa

Muhtasari
  • Mwanasosholaiti Vera Sidika ni miongoni mwa watu maarufu ambao walifahamika sana siku zile kwa kuishi maisha ya kifahari
Image: INSTAGRAM// VERA SIDIKA

Mwanasosholaiti Vera Sidika ni miongoni mwa watu maarufu ambao walifahamika sana siku zile kwa kuishi maisha ya kifahari.

Wengi walidai kwamba Vera alikuwa anawachumbia Sponsors kabla ya kuolewa na msanii Brown Mauzo.

Mwaka jana mwanasosholaiti huyo alibarikiwa na mtoto, anayefahamika kama Asia na mwenye urembo wa kipekee.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram, mmoja wa mashabiki wake alimuuliza ushauri wwake kwa wasichana ambao wanawachumbia wababa.

Ni tabia au mtindo wa wasichana wadogo kuchumbiana na akina baba ambao wana umri wa baba yao kwa ajili ya pesa.

Ndio walikuwa wanawaita 'sponsors'lakini wamewabadilisha majina na kuanza kuwaita 'wababa'.

Huku akijibu swali hilo, Vera aliwahimiza au kuwashauri wasichana hao wanyonye pesa za wababa lakini waweze kuwekeza.

"Ushauri wako kwa msichana anayechumbia wababa,"Shabiki aliuliza.

"Kula pesa yake mzuri, lakini cha muhimu wekeza,"Alijibu Vera.