"Tuma pesa mtoto anataka kuenda coast", Wahu amjibu Nameless kwa utani

Wanandoa hao walitangaza wiki jana kuwa wanatarajia mtoto wao wa tatu hivi karibuni.

Muhtasari

• Nameless ambaye yuko Marekani kimuziki alitaka kujua nini kinaendelea nchini Kenya.

• Mkewe Wahu alimjibu kwamba mtoto ujauzito umempa hisia za kutaka kuenda pwani kwa hiyo atume pesa

Wanandoa maarufu nchini Kenya ambao pia ni wasanii, Nameless na mkewe Wahu Kagwi hawaishi vituko vya ucheshi mitandaoni kila kukicha, na hili limewazolea umaarufu mkubwa kutoka kwa watumizi wa mitandao ya kijamii.

Katika moja wapo ya utani ambao wapenzi hao wawili wanafanyiana kwenye mtandao wa Facebook, msanii Nameless ambaye yupo nchini Marekani kwa ziara ya kimuziki alitaka kujuzwa ni nini kwa sasa kinachozungumziwa nchini Kenya.

Akizua utani wa kutumia kauli ya ‘Tingiza Miti’ iliyokuwa ikisikika wakati mgombea urais, wakili msomi George Wajackoyah alipokuwa akizindua rasmi manifesto yake, aliwataka mashabiki wake nchini kumjuza nini kingine kinaendelea kwqa sababu ako mbali kidogo na nyumbani.

“Kwa hiyo tumeamua ni kutingiza miti ama? Nijuze, niko mbali kidogo!” aliandika Nameless kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Mkewe, Wahu Kagwi ambaye wiki iliyopita walitangaza kutarajia mtoto wa tatu aliachia maoni yake kwenyeukurasa huo huku akimtaka Nameless kutuma pesa za kupeleka mtoto ziara pwani.

Wahu aliachia kauli hiyo kwa nia ya utani huku akiwazua muktadha wa vitu wanavyovifanya wanawake wajawazito ambavyo si vya kawaida.

“Ati utume pesa za vacation mtoi anataka kwenda coast,” Wahu alijibu kwa utani mkubwa.

Juzi kati wawili hao walizua jingine kwamba mtoto wao Nyakio ambaye sasa anaelekea kunyang’anywa mamlaka ya kuwa kitinda mimba na yule mtarajiwa alitaka kujua jina lake la kiingereza na kuwataka wana mitandao kuwasaidia.

Nameless na Wahu wamekuwa kwenye ndoa kwa zaidi ya miaka kumi na wanatajwa kuwa miongoni mwa watu maarufu wachache wanaodumu kwenye ndoa, mpaka kufikia hatua ya kutajwa mara kadhaa kuwa wanandoa maarufu nchini Kenya.

Nameless aliondoka nchini wiki moja iliyopita kwenda ziara ya kimuziki Marekani, punde tu baada ya kuweka wazi kwa umma kwamba ni rasmi wanatarajia mtoto wa tatu hivi karibuni.

Wengine walisema kwamba msanii Nameless amekwepa kujipata katika mtafaruku wa mabadiliko ya kihisia ya mara kwa mara kutoka kwa mkewe, jambo ambalo ni kawaida sana kwa wanawake wajawazito ambao huwa wanabadilika hisia ghafla na kuhitaji vitu fulani visivyomithilika kwa wakati huo huo.