Sijawai kula pesa ya mitandao,Ex wangu aliiba akaunti yangu ya Instagram-Mustapha

Kanali alisema kuwa uhusiano wake na Notiflow ulimwangusha sana na kumuua kimuziki, Notiflow aliiba akaunti yake ya Instagram.

Muhtasari
  • Kanali alisema kuwa uhusiano wake na Notiflow ulimwangusha sana na kumuua kimuziki, Notiflow aliiba akaunti yake ya Instagram.
Msanii mkongwe kutoka Ogopa Djs, Coonel Mustafa
Msanii mkongwe kutoka Ogopa Djs, Coonel Mustafa
Image: Colonel Mustafa (Instagram)

Mmoja wa watu mashuhuri maarufu wa Kenya katika tasnia ya muziki Kanali Mustapha amerejea tena baada ya miaka kadhaa yakutotoa muziki.

Akiongea kwenye mahojiano na Amina Abdi Rabar, Colonel alisema kuwa mpenzi wake wa zamani ndio sababu iliyomfanya aingie kwenye tasnia ya muziki na ndiye aliyesababisha anguko lake.

Kanali alisema kuwa uhusiano wake na Notiflow ulimwangusha sana na kumuua kimuziki, Notiflow aliiba akaunti yake ya Instagram.

Mustapha alisema kuwa alipoteza simu na aliamua kuingia kwa kutumia akaunti ya Notiflow ya Instagram na hakutoka, hivyo Notiflow alipata akaunti yake ya Instagram na kubadilisha kila kitu na kuibadilisha kuwa ukurasa wake wa kmashabiki wake.

"Uhusiano wangu na Notiflow haukuwa wa kufurahisha, yaani sikuwa na furaha, aliiba akaunti yangu ya Instagram akaimiliki, nilipotea simu nikaamua kutumia simu yake, hapo ndipo alipata nafasi ya kuiba akaunti yangu."

Huku akizungumzia muziki na kurejea kwake Mustapha aliwasihi mashabiki na wanamitandao kumuunga mkono katika safari yake.

Colonel alisema kuwa amekuwa akijaribu kuweka mawazo yake pamoja na sasa amerejea kwenye tasnia ya muziki na anajua ataua.

"Sijawahi kula pesa ya mitandao ya kijamii, lakini nawasihi na kuomba mashabiki wangu waniunge mkono kwani nimerejea."