"Mama nimefanikiwa!" Zari Hassan afichua jambo analojivunia zaidi maishani

Pinto alijiunga na chuo kikuu nchini Afrika Kusini mwaka huu baada ya kufuzu mwaka jana

Muhtasari

•Pinto Tale ambaye ni mzaliwa wa kwanza wa Zari alijiunga na chuo kikuu nchini Afrika Kusini mwaka huu baada ya kufuzu mwaka jana.

•Zari alijawa na fahari kubwa baada ya mwanawe kukamilisha masomo yake ya chuo na kufuzu kujiunga na chuo kikuu.

katika karamu iliyofanyika wikendi
Zari Hassan na wanawe Pinto na Raphael katika karamu iliyofanyika wikendi
Image: INSTAGRAM// ZARI HASSAN

Mwanasoshalaiti Zari Hassan amebainisha kuwa kumuona mwanawe katika chuo kikuu ni jambo ambalo anajivunia zaidi.

Pinto Tale ambaye ni mzaliwa wa kwanza wa Zari alijiunga na chuo kikuu nchini Afrika Kusini mwaka huu baada ya kufuzu mwaka jana

Mama huyo wa watoto watano alishindwa kuficha furaha yake baada ya kuhudhuria karamu na marafiki wa mwanawe.

"Hili ndilo jambo ambalo najivunia zaidi, kuwa na mvulana wangu katika chuo kikuu. Mama nimefanikiwa," Zari aliandika chini ya video iliyoonyesha mwanawe akijivinjari pamoja ma marafiki zake ambayo alipakia kwenye Instastori zake.

Zari alijumuika na mwanawe pamoja na kundi kubwa la marafiki zake katika karamu iliyofanyika wikendi.

Mtoto wake wa pili Raphael Junior pia ni miongoni mwa waliohudhuria karamu hiyo ambayo washiriki wake wengi walikuwa vijana.

"Marafiki wakubwa zaidi," Mwanasoshalaiti huyo aliandika chini ya video za karamu hiyo alizopakia.

Pinto ambaye ni mtoto wa Zari na aliyekuwa mumewe Ivan Semwanga alifuzu kuingia chuo kikuu mwaka jana.

Zari alijawa na fahari kubwa baada ya mwanawe kukamilisha masomo yake ya chuo na kufuzu kujiunga na chuo kikuu.

"Mehhn, mama pekee ndiye anayeweza kuelewa. Mwanangu ataenda chuo kikuu mwaka ujao," Aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Licha ya kupita mitihani yake Pinto pia alikuwa makamu wa rais, nahodha wa raga, mwanaspoti bora wa mwaka katika chuo ambacho alikuwa, jambo ambalo mamake alijivunia.

Mapema mwaka huu mpenzi huyo wa zamani wa Diamond Platnumz alimteua Pinto kuwa mkurugenzi katika Chuo chake cha Brooklyn City.