"Nitaolewa tena, mwisho wa mwaka huu nitakuwa mjamzito" - Esma Platnumz

Mwanadada huyo alisema tayari yupo kwenye mahusiano baada ya awali kuvurugika.

Muhtasari

• Alidokeza kwamba mwisho wa mwaka huu atakuwa na ujauzito na kuzaa kwani anampenda sana huyo mchumba wake wa sasa.

Mjasiriamali Esma Khan, dada mkubwa msanii Diamond Platnumz
Mjasiriamali Esma Khan, dada mkubwa msanii Diamond Platnumz
Image: Instagram

Dadake msanii Diamond Platnumz, Esma Platnumz hatimaye amezungumzia suala la kujaribu ndoa tena, miaka michache baada ya ndoa yake kuvunjika na mfanyibiashara mkwasi kutoka taifa la Afrika Kusini.

Esma Platnumz alikuwa ameolewa kaam mke wa tatu na mfanyibiashara huyo mwenye asili ya Kitanzania anayepiga madili yake nchini Afrika Kusini kwa jina Msiswa ambapo mahusiano hayo hayakuwa na tija na kufikia kikomo miaka miwili iliyopita.

Akifunguka kuhusu kujaribu ndoa tena kupitia mahojiano ya kituo kimoja cha habari nchini humo, Esma alisema ni kweli ako na mchumba na wanatarajia hivi karibuni kufanya ndoa.

“Ndio, niko kwenye uhusiano. Lakini uhusiano wangu hivi sasa sio wa mitandao ya kijamii kama hapo awali. Yeye ni mchapakazi na ana akili kila wakati na sura yake ni ya kufa. Yeye pia ni rafiki. Siwezi kudate na mtu ambaye hawezi kuniinua,” Esma alitamba kwenye mahojiano hayo.

Vile vile mwanamke huyo ambaye pia anajiongeza kama mjasiriamali alisema anatarajia kupata mtoto na mchumba huyo wake ambaye kwa sasa amemweka faraghani na kusema mipango yote ipo kwenyewe, kabla ya mwisho wa mwaka huu kila kitu kitaitikia.

“Niko kwenye uhusiano mzuri na ninatamani sana kuolewa tena. Nampenda sana. Ninapata mtoto naye na mipango yote inaendelea. Mwishoni mwa mwaka huu, nitakuwa mjamzito tutazaa mtoto wetu wa kiume, hata wa kike yeyote atakayekuja,” Esma alisema kwa furaha.

Esma alizua mjadala baada ya kusema kwamab aliavya ujauzito wa mwanaume wake wa kwanza baada ya kutengana kwa kile alichokisema kwamba hakuna vile angekubali kuzaa mtoto na mwanaume ambaye tayari hisia zake zilishafukiwa, na hivyo hata angemzaa yule mtoto basi hangempenda na angeishi naye kwa majuto.