Mbuzi akamatwa na polisi kwa tuhuma za wizi wa kimabavu

Watu walisema mbuzi huyo alikuwa ni mshirikina aliyejigeuza mbuzi ili kukwepa adhabu

Muhtasari

• Ilisemekana wezi wa magari walikuwa wawili na baada ya jaribio lao kutibuliwa, mmoja akatoroka na aliyekamatwa akageuka kuwa mbuzi.

Mbuz
Mbuz
Image: The Star

Je, unafahamu kwamba jela si tu za binadamu bali hata Wanyama hukamatwa na kutiwa korokoroni kwa makosa mbali mbali kama vile Wanyama?

Kama huamini hilo basi unafaa kuanza kuamini kwani kuna matukio mbali mbali ambayo yametokea na kuripotiwa kwenye vyombo vya habari kuhusu Wanyama kukamatwa na kutiwa kwenye seli kisa makosa ya uhalifu.

Katika visa vingi vya wanayama kukamatwa na polisi kwa tuhuma za uhalifu, kisa kilichozungumziwa zaidi ni kile kilichotokea nchini Nigeria miaka kadhaa iliyopita ambapo mbuzi alitiwa nguvuni na jeshi la polisi kwa tuhuma za wizi wa kimabavu.

Nchini humo, watu wengi wanaaminia sana katika uganga na kukamatwa kwa mbuzi huyo wengi waliamini ni mtu mwizi ambaye aliwawekea watu kifumba macho ili kumuona kama mbuzi na hilo ndilo lilipelekea mbuzi huyo kutiwa korokoroni.

Katika taarifa hizo za kuchekesha na kuchanganya kwa wakati mmoja zilizochapishwa kwenye majarida mbalimbali ndani na nje ya taifa hilo, polisi washika doria walimpeleka mnyama huyo mwenye madoadoa meusi na meupe kwa polisi wakisema kuwa ni jambazi mwenye silaha ambaye alitumia uchawi kujigeuza mbuzi ili kukwepa kukamatwa baada ya kujaribu kuiba gari.

"Kikundi cha watu walinzi walikuja kuripoti kwamba walipokuwa kwenye doria waliona baadhi ya watu waliokuwa wakijaribu kuiba gari. Wakawafuata. Hata hivyo mmoja wao alitoroka huku mwingine akigeuka kuwa mbuzi,” jarida la Reuters lilinukuu taarifa za polisi wa Nigeria.

Kulingana na taarifa kutoka nchini humo, mkuu wa polisi alidhibitisha kwamba mbuzi yupo kizuizini kwenye seli ila akasema kwamba bado hawangeweza kudhibitisha hadithi hiyo kwamba huyo ni binadamu aliyejigeuza mbuzi kwani jambo hilo linafaa kudhibitishwa tu na wanasayansi na wala si kwa macho ya kawaida tu.

Imani katika uchawi imeenea katika sehemu nyingi za Nigeria, taifa lenye watu wengi zaidi barani Afrika. Wakazi walifika katika kituo cha polisi kumwona mbuzi huyo, aliyepigwa picha kwenye gazeti moja la kitaifa akiwa amepiga magoti karibu na rundo la majani.