(+video) "Serikali ina mkono mrefu" Jamaa amuomba polisi kusaidia kupata ufunguo uliopotea

Mwanaume huyo anasisitiza kwamba sababu serikali ina mkono mrefu basi polisi ataupata ufunguo ule.

Muhtasari

• “Mkubwa! Habari yako, funguo zangu zimanguka kwa nyumba na huwa nasikia serikali ina mkono mrefu, unaweza kuja kunisaidia kutoa,” mwanaume huyo anauliza polisi

Mchekeshaji Captain Otoyo amepakia video kweney ukurasa wake wa Instagram ikionesha mwanaume akimfuata afisa wa polisi aliyekuwa akichunga benki moja jijini huku akimuambia kwamba ufunguo wake aliufungia kwa nyumba na kumtaka polisi huyo kumsaidia.

Mwanaume huyo aliyeonekana kutokuwa na woga anamkaribia polisi na kumuomba amsaidie kutoa ufunguo wake kwa nyumba kwa kile alisema kwa utani kwamba huwa anasikia serikali ina mkono mrefu.

“Mkubwa! Habari yako, funguo zangu zimanguka kwa nyumba na huwa nasikia serikali ina mkono mrefu, unaweza kuja kunisaidia kutoa,” mwanaume huyo anauliza polisi huyo ambaye ako katika shughuli yake ya kulinda benki eneo la kutolea pesa la ATM.

Polisi huyo kwa ghadhabu anamuamrisha jamaa huyo kuondoka huku akisisitiza kwamab kwa sababu serikali ina mkono mrefu inaweza fikia ufunguo ule ulioanguka kwa nyumba kulingana na yeye na kumtolea nje.

Polisi anamalizia kumsuuma kwa kumpiga kumbo jamaa huyo.