Zari Hassan hatimaye afichua umri wa mpenzi wake wa sasa

Mpenzi huyo wa zamani wa Diamond alibainisha kuwa mpenziwe sio mdogo kama jinsi wakosoaji wake wamekuwa wakidai.

Muhtasari

•Mpenzi huyo wa zamani wa Diamond alibainisha kuwa mpenzi wake sio mdogo kama jinsi wakosoaji wake wamekuwa wakidai.

•Zari alifichua kuwa kuna baadhi ya watu ambao wamekuwa wakiunga mkono mahusiano yake na kuyathamini.

Image: INSTAGRAM// ZARI HASSAN

Mwanasoshalaiti maarufu  Zari Hassan amewasuta watu wanaomkosoa kwa kuchumbiana na mwanaume ambaye ni mdogo kuliko yeye.

Zari amesema kuwa mwanamke yeyote yupo huru kuwa kwenye mahusiano na mwanaume aliyepiku kwa umri kama vile tu sio kosa kwa mwanaume kuchumbiana na mwanamke mwenye umri mdogo kumliko.

"Mbona mwanaume  akichumbiana na mwanamke mdogo ni sawa lakini mwanamke na ikiwa kinyume jamii sio sawa kwa jamii," Zari alihoji katika video ambayo alipakia kwenye mitandao ya kijamii.

Katika video hiyo, mama huyo wa watoto watano alibainisha kuwa mpenzi wake sio mdogo kama jinsi wakosoaji wake wamekuwa wakidai.

Alifichua kuwa amempiku mpenzi wake wa sasa ambaye jina lake bado halitambulishwa  kwa takriban miaka kumi.

"Mpenzi wangu sio mdogo. Ana miaka 30 anaelekea 31 Desemba mwaka huu. Yeye sio mdogo, anakaa mdogo. Mimi natimiza miaka 42 mwaka huu na huwezi kujua," Alisema.

Aliongeza "Kama hunijui na unione na Latifah utadhani kuwa huyo ndiye mtoto pekee niliye naye. Lakini inakaa mimi ni mzee kwa kuwa niko na watoto na kusahau kuwa baadhi yetu tulizaa tukiwa wadogo."

Licha ya kuwa na halaiki ya wakosoaji nyuma yake, mpenzi huyo wa zamani wa Diamond Platnumz alifichua kuwa kuna baadhi ya watu ambao wamekuwa wakiunga mkono mahusiano yake na kuyathamini.

Takriban mwezi mmoja uliopita, mwanasoshalaiti huyo aliweka wazi kuwa maisha yake hayafungwi na jamii na kubainisha kuwa ana haki kamili ya kumchagua yule ambaye angependa kuchumbiana naye.

"Ukiniambia nichumbie nani na nisichumbie nani, nawajua wa aina hizo. Lakini hapa ndipo ninapoamua kubaki. Ni nini kinachokufanya ufikiri kwamba watu wengine hawana hadhi?,"  Zari alisema.

Mzaliwa huyo wa Uganda anayeishi Afrika Kusini kwa sasa aliwataka watu kusita kuhoji kuhusu kazi na uwezo wa kifedha wa mpenziwe.

Aidha alibainisha kuwa uamuzi wa nani wa kuchumbiana uko kwake na sio kwa wale ambao wanakosoa hatua zake.

"Niko hapa kwa sababu nataka kuwa hapa, sio kwa sababu mnataka kunichagulia mahali pa kuwa," Alisema.

Kabla ya kujitosa kwenye mahusiano na mpenziwe wa sasa, Zari alichumbiana na mfanyibiashara wa Uganda aliyetambulishwa kama GK Choppa. Hayo yalitokea mapema mwaka huu.