"Napendelea ilifanyika hivo!" Amber Ray afunguka kuharibika kwa ujauzito wake na Jimal

Mwanasoshalaiti huyo alidokeza kuwa mahusiano yake na Jimal yalianza kusambaratika baada ya kuwa mjamzito.

Muhtasari

•Amber Ray alisema wakati alijitosa kwenye mahusiano na Jimal, mfanyibiashara huyo alikuwa amemhakikishia kwamba yeye na mkewe Amira walikuwa wakitalikiana.

•Mwanasoshalaiti huyo alifichua kuwa ujauzito ambao alikuwa ameubeba haukutimia kwani uliharibika katika kipindi hicho.

Amber Ray na Jimal Rohosafi
Amber Ray na Jimal Rohosafi
Image: INSTAGRAM

Mwanasoshalaiti Faith Makau almaarufu Amber Ray amefichua kuwa mfanyibiashara Jimal Rohosafi alimpachika ujauzito wakati walipokuwa kwenye mahusiano

Wawili hao walijitosa kwenye mahusiano ya kimapenzi mapema mwaka jana  ila wakatengana  mwezi Januari mwaka huu.

Katika kipindi cha 'AS IT IS' kwenye YouTube Channel yake, Amber Ray alidokeza kuwa mahusiano yake na Mwenyekiti huyo  wa Muungano wa Wamiliki wa Matatu Nairobi yalianza kusambaratika baada yake kuwa mjamzito

"Hapo ndipo kila kitu kilipodhihirika kwani baada ya hapo ndipo alipopost mke wake na watoto. Nilihisi kama kuna kitu hakikuwa sawa," Amber Ray lisema katika mazungumzo na Shicco Waweru.

Mama huyo wa mvulana mmoja alieleza kuwa wakati alipokuwa akijitosa kwenye mahusiano na Jimal, mfanyibiashara huyo alikuwa amemhakikishia kwamba yeye na mkewe Amira walikuwa wakitalikiana.

"Mbona upost mtu ambaye unatalikiana naye? Nilikuwa napitia mengi," Alihoji.

Mwanasoshalaiti huyo alifichua kuwa ujauzito ambao alikuwa ameubeba haukutimia kwani uliharibika katika kipindi hicho.

Hata hivyo alidokeza kwamba  hakujuta kuwa ilifanyika kwani hakuwa tayari kumlea mtoto ambaye angezaliwa pekee yake.

"Napendelea kuwa ilifanyika hivo kwani sidhani nitawahi kuwa na nguvu ya kuwa mama single katika maisha yangu kwani kwa hali nzima, hakuna njia ambayo tungeweza kuishia pamoja," Alisema Amber.

 Mwanasoshalaiti huyo alibainisha kuwa mahusiano yake na Jimal Rohosafi yalikuwa makosa na hayakustahili.

"Kilichofanyika kilifanyika na tunasonga mbele licha ya yote," Alisema

Amber Ray tayari ana mtoto mmoja mwenye umri wa miaka 9 kutoka kwa mahusiano yake ya hapo awali

Amber Ray alifichua kuwa alimpata mwanawe Gavin akiwa na umri wa takriban miaka 18.

Alieleza  kuwa hakupanga kupata mtoto akiwa na umri huo mdogo.