"Simtaki Mond" - Wema Sepetu amkana Diamond, amtaka Jeshi

Sepetu alikuwa akizungumza Dodoma katika hafla ya ufunguzi wa mgahawa wa Shishi Foos.

Muhtasari

• Itakumbukwa Wema Sepetu aliwahi kuwa katika mahusiano na msanii Diamond Platnumz kwa muda mrefu.

Sepetu alimkana Diamond hadharani na kusema mbadala wake awe Harmonize
Sepetu alimkana Diamond hadharani na kusema mbadala wake awe Harmonize
Image: Instagram

Wikendi iliyopita, mwanamuziki na muigizaji Shilole ambaye pia ni mjasiriamali alikuwa anafungua tawi la mgahawa wake jijini Dodoma, Shishi Food.

Katika hafla hiyo kubwa ya ufunguzi, aliwaalika watu maarufu mbali mbali ambapo jukwaa lilikuwa limefurika hadi pomoni.

Mwigizaji Wema Sepetu alikuwa mmoja wa wale waliopanda jukwaani kutoa maneno yao ya kuibariki biashara ya mwanadada mwenzake Shilole.

Wema alipokuwa akizungumza na mashabiki, walimtaka aimbe japo wimbo mmoja na wengi walikuwa wanamtaka aimbe wa Diamond, aliyekuwa mpenzi wake na wengine walikuwa wanamtaka aimbe wimbo wa Harmonize.

Itakumbukwa Wema Sepetu aliwahi kuwa katika mahusiano na msanii Diamond Platnumz kwa muda mrefu ambao mahusiano yao mpaka sasa hivi yanafagiliwa sawa kutokana na utu uzima waliionesha hata baada ya kuachana, hawakupalilia chuki baina yao.

Cha kushangaza ni kwamba Wema alikataa wazi wazi kwamba yeye hamtaki Diamond na hawezi kuimba wimbo wake, na badala yake akadokeza kwamab angependa kuimba wimbo wa Jeshi, jina la kimajazi la Harmonize.

“Nyinyi mnataka Diamond, basi mimi simtaki Mond, njoo tupigane. Namtaka Jeshi,” Wema Sepetu alinukuliwa akiwa jukwaani huku watu wanamshangilia kwa kumtaka atumbuize kwa wimbo.