(+video) Pastor Ng'ang'a awapa wanandoa zawadi ya gari dogo, awatania eti ni pikipiki

Video hiyo akiwabariki wanandoa na gari dogo aliloliita Pikipiki ilipakiwa kwenye Facebook ya Sasa TV.

Muhtasari

• Ng'ang'a alisema kwamba waumini hao walienda kwa ajili ya maombi na kumwaambia walitumia usafiri wa matatu ndipo aliamua kuwapa zawadi.

• Awali aliwatania kwamba ni piki piki alikuwa anawapatia ndio mwishowe wakagundua ni gari.

Mchungaji mwenye utata mwingi, James Ng’ang’a wa kanisa la Neno kwa mara nyingine amezua mjadala mitandaoni baada ya video kuibuka akijitolea kumpa mmoja wa waumini wake zawadi ya gari zee.

Katika video hiyo ambayo ilipakiwa kwenye ukurasa wa Facebook wa kituo chake cha runinga, Sasa TV, mchungaji Ng’ang’a alielezea jinsi alimjua muumini huyo pamoja na mke wake.

Mwanzo aliwatania kwamba alikuwa anwapa zawadi ya pikipiki na mpaka kuwapa wazee wa kanisa ufunguo ili kuelekea na waumini hao wanandoa nje kuwakabidhi zawadi ya ‘pikipiki’ zawadi ambayo baadae waligundua ni gari la kitambo ambalo mchungaji Ng’ang’a alikuwa amekarabati.

“Kuna rafiki yangu mmoja amekuwa anatembea na gari la matatu, juzi amekuja maombi nikamuuliza amekuja na nini akasema matatu, sasa nikasema acha nimpe kapikipiki,” Ng’ang’a alisema huku akiwaita kujongea mbele ili kupokezwa ufunguo wa zawadi.

“Wacha nimpatie pikipiki atembee nayo. Ni heri pikipiki kwa sababu si italala kwako kuliko kuenda kwa matatu,” Ng’ang’a aliongeza.

Wandoa hao wakongwe waliongozana na wazee kuenda nje eneo magari yalikuwac yameegezwa na kushangaa walipogundua kwamab ni gari walikuwa wamepewa na mchungaji na wala si piki piki kama ambavyo aliwatania kanisani.

Kwa mbwembwe tele, mchungaji Ng’ang’a aliwafuata huku kanisa likiimba na kuwaambia kwamba hilo gari ndilo alikuwa anawapa kama piki piki ya kutembelea na kuasi matumizi ya magari ya uchukuzi wa umma.