"Nakupenda babe!" Diamond afurahi baada ya bintiye Tiffah kujivunia kufanana naye

"Nafanana na baba yangu, amini hilo!" Tiffah alisema.

Muhtasari

•Katika video hiyo ambayo Diamond alipakia kwenye Instagram, Tiffah alisikika akijivunia kuwa anafanana na babake.

•Diamond alimhakikishia bintiye huyo wa pekee kuhusu upendo wake mkubwa kwake.

Image: INSTAGRAM// DIAMOND PLATNUMZ

Staa wa Bongo Diamond Platnumz akiwa alifurahi baada ya bintiye na aliyekuwa mpenzi wake Zari Hassan, Tiffah Dangote kurekodi video akiongea na kuikarabati kuonyesha kana kwamba ana ndevu.

Katika video hiyo ambayo Diamond alipakia kwenye Instagram, Tiffah alisikika akijivunia kuwa anafanana na babake.

"Nafanana na baba yangu, amini hilo!" Tiffah alisema katika video hiyo ambayo ilirekodiwa kwa kutumia FaceApp.

Malkia huyo mwenye umri wa miaka saba alikuwa akizungumza na mama yake Zari kwenye video hiyo fupi.

"Hii ni sura ya baba" alimwambia.

Zari alisikika akimueleza bintiye kuwa  mwonekano huo wa sura yake uliokarabatiwa ni toleo lake jingine.

Huku akijibu video hiyo, Diamond alimhakikishia bintiye huyo wa pekee kuhusu upendo wake mkubwa kwake. 

"@princess_tiffah nakupenda babe," Diamond alimwandikia bintiye.

Image: INSTAGRAM// DIAMOND PLATNUMZ

Tiffah ni mtoto wa kwanza wa bosi wa WCB Diamond Platnumz. Alizaliwa mnamo Novemba 6, 2015 wakati staa huyo wa bongo  alikuwa kwenye mahusiano na Zari.

Katika kipindi cha mahusiano yao, wasanii hao wawili wa Afrika Mashariki walibarikiwa na mtoto mwingine mmoja pamoja, Prince Nillan ambaye alizaliwa Desemba 6, 2016.

Mara nyingi Diamond ameonekana kuwapendelea watoto wake na Zari zaidi ya watoto wake wengine wawili wanaojulikana. Mwanamuziki huyo ana watoto wengine pamoja na Hamisa Mobetto na Tanasha Donna.

Mwezi jana Zari aliweka wazi kuwa anashirikiana vizuri na  mpenzi huyo wake wa zamani katika malezi ya watoto wao wawili.

Katika mahojiano na Wasafi Media, Zari alifichua kuwa yeye na Diamond wamekuwa wakijadiliana mara kwa mara kuhusu njia bora ya kuwalea watoto wao.

"Tumefanya malezi ya kushirikiana kuwa rahisi sana. Tumekuja pamoja na kusema tunataka bora zaidi kwa watoto wetu,tunaketi na kuongea," Zari alisema.

"Tuna maslahi yao bora moyoni; wanataka nini?  wanataka kuenda wapi? wanajiona wapi?"

Mzaliwa huyo wa Uganda alibainisha kuwa kuelewana kuzuri kwake na Diamond kumerahisisha ushirikiano wao katika malezi.

Alidokeza kuwa uhusiano wao wa sasa umekuwa mkubwa zaidi ya wakati ambapo walikuwa kwenye mahusiano.

"Nadhani imekuwa rahisi kwa sababu sasa tunaelewana zaidi, sio kama wapenzi lakini tunaelewana kama wazazi na marafiki. Mimi na Diamond kwa sasa hivi tumekuwa marafiki zaidi ya jinsi tulivyokuwa wapenzi. Inafanya mambo kuwa rahisi kwetu," Alisema.

Zari na Diamond walitengana mwaka wa 2018 baada ya kuwa kwenye mahusiano kwa takriban miaka minne.