Diamond adokeza kuhusu kufunga ndoa hivi karibuni

"Nami niko njiani InshaAllah," Diamond alisema.

Muhtasari

•Diamond alidokeza hayo wakati akimpongeza msemaji wa Yanga FC Haji Manara kwa kufunga ndoa yake ya nne.

•Si mara ya kwanza kwa Diamond kudokeza kuhusu kufunga ndoa hivi karibuni.

Image: INSTAGRAM// DIAMOND PLATNUMZ

Huenda tukashuhudia staa wa Bongo Diamond Platnumz akifunga pingu za maisha na mpenzi wake asiyejulikana hivi karibuni.

Msanii huyo ambaye ni baba huyo wa watoto wanne wanaojulikana amedokeza kuwa atafanya harusi siku ambayo hajabainisha.

Diamond alidokeza hayo wakati akimpongeza msemaji wa Yanga FC Haji Manara kwa kufunga ndoa yake ya nne.

"Nami niko njiani InshaAllah," aliandika chini ya chapisho la Manara la kumtambulisha mkewe kwa wanamitandao.

Bosi huyo wa WCB alikuwa akicomment kwenye chapisho la Manara kwenye Instagram ambapo alimtambulisha mke wake mpya Ruush Bugati na kumshukuru Maulana kwa harusi yao ambayo ilifanyika wikendi.

"Hasbuna llahu Waniimal Wakiil.Bismillah MashaAllah 🙏🏻Kwa sasa Mke wangu anafahamika kama @ Ruush Bugati ❤️❤️," aliandika Manara.

Manara hata hivyo alionekana kutilia shaka suala la Diamond kufuata nyayo zake na kufunga ndoa hivi karibuni.

"Diamond Platnumz ukioa karibuni njoo Rotana uniite Jibwa," msemaji huyo wa Yanga alimjibu Diamond.

Si mara ya kwanza kwa Diamond kudokeza kuhusu kufunga ndoa hivi karibuni. 

Kwa kipindi kirefu mwaka huu, staa huyo wa Bongo amekuwa akionyesha dalili za kupiga hatua hiyo muhimu ila bado hajaweka wazi mwanamke ambaye ameuteka moyo wake na kufanya awe tayari kufunga pingu za maisha.

"Nitafunga ndoa wakati wowote hivi karibuni. Hatuwezi kujuua. Ni Mungu hupanga yote, sisi hutamani tu kama binadamu lakini Mungu ndiye hupanga kila kitu," alisema katika mahojiano na DW Afrika mwezi Julai.

Wakati wa mahojiano hayo, Diamond hata hivyo alieleza hofu yake kuwa ndoa huenda ikazorotesha taaluma yake ya muziki.

Diamond hajakuwa kwenye mahusiano au ndoa yoyote  inayojulikana wazi tangu mwaka wa 2020.

Hata hivyo, miezi ya hivi majuzi amekuwa akionyesha wazi kwamba kuna malkia mpya kwenye ufalme wake