Mchekeshaji wa Churchill, Nusra Yusuf akanusha madai kuwa alighushi bili ya chakula

Haya ni baada ya watu kumsuta kuwa alipakia risiti ya bili ya chakula ambayo ilipakiwa mwaka jana na Vera Sidika.

Muhtasari

• Nasra alijigamba na kusema chakula cha elfu 59 hakihitaji kuliwa na haraka ndio maana alikuwa anamalizia kula baada ya saa hizo.

• Mcheshi huyo alisema kuwa hoteli hiyo imemkosea heshima na kuwakosea pia wateja wake kwa kumpa risiti ambayo sio yake.

Nasra Yusuf
Image: Nasra Yusuf

Mchekeshaji Nasra Yusuf amekanusha madai kuwa risiti aliyoweka mtandaoni akiwa hotelini kuonyesha staftahi yake aliyokuwa anakula ilimgharimu elfu 59 na 200 sio yake.

Wanamitandao waliunganisha risiti hiyo ya Nasra na aliyoiweka mwanasosholaiti Vera Sidika mwaka uliopita ya mwezi wa June.

Risiti hiyo aliyoipakia Yusuf ilionesha uwuiano katika kila kitu na risiti ya Sidika ya mwaka jana kutoka tarehe hadi kiasi cha pesa ambazo chakula hicho cha asubuhi kiliwagharimu wote.

Nasra amekataa madai hayo na kusema hoteli hiyo ilimpa risiti ya mwaka jana ambayo sio yake ila bado anasisitiza kuwa alitumia elfu 59 kwa staftahi yake.

Aliiweka picha hiyo na kuandika "Staftahi yangu ya leo. Elfu 59, 200 na bado nahesabu. Sasa 59,200 ni kitu ya kuniambia nadanganya kweli,"alisema.

Mcheshi huyo alisema kuwa hoteli hiyo imemkosea heshima na kuwakosea pia wateja wake kwa kumpa risiti ambayo sio yake.

Alisema kuwa alikula staftahi yake kwa muda wa saa tano sasa, kutoka saa tatu asubuhi amekuwa akila chakula chake hicho cha elfu 59.

Nasra alijigamba na kusema chakula cha elfu 59 hakihitaji kuliwa na haraka ndio maana alikuwa anamalizia kula baada ya saa hizo.

Aliongeza na kusema kuwa baada ya kula chakula hicho ataenda kula chakula chake cha mchana cha elfu 200.

Baadaye, mcheshi huyo alisema kuwa anatafuta wakili mzuri ili aweze kuishtaki hoteli hiyo kwa kumpa risiti hiyo.

Mwezi wa Juni, mcheshi huyo na mume wake Rashid walimpoteza manawe aliyefariki kabla ya kuzaliwa.

Mchekeshaji huyo alisema kwamba alipoteza zawadi yake kabla hata ya kuipokea mikononi licha ya kuweka maandalizi mazuri kutoka jina, nguo na kila kitu kinachohitajika katika maandalizi ya kumpokea mtoto anapozaliwa.

Katika hali ya kujipa tumaini, Yusuf pia alisema kwamba alifurahia kwamba aliishi na ujauzito huo hadi kuifahamisha familia, ndugu , jamaa na marafiki kuhusu ujio wake, japo safari hajaikamilisha kama walivyotarajia wengi kumuona.