Mwanasosholaiti afariki akifanyiwa upasuaji wa Liposuction nchini India

Katika video ya kutatiza macho inayosambazwa mitandaoni, mwili wa sosholaiti huyo unaonekana ukiwa umekufa ganzi na daktari anasikika akimhurumia.

Muhtasari

• Katika video iliyorekodiwa muda mfupi baada ya kufa, daktari alisikika akimwomba msamaha.

Mwanasosholaiti Amelia Pounds afariki akifanyiwa upasuaji wa liposuction
Mwanasosholaiti Amelia Pounds afariki akifanyiwa upasuaji wa liposuction
Image: Instagram

Liposuction ni upasuaji wa kupunguza ufuta katika sehemu ya utumbo wa chini. Ni upasuaji wa kuongeza urembo amabo umekumbatiwa sana na wanadada wengi ambao wanathamini mionekano yao, wengi wakiwa wale wanaotaka kuwa na viuno laini na vyembamba kama nyigu.

Nchini Nigeria Sosholaiti, Amelia Pounds, ameripotiwa kufariki dunia nchini India alipokuwa akifanyiwa upasuaji huo wa liposuction, ambao ulimwendea mvange.

Katika video ambayo imekuwa ikisambazwa mitandaoni, mwanasosholaiti huyo anaonekana amezima kabisa na mwili wake kugeuka gogo tu lisoloweza kujisogeza.

Amelia Pounds ni mwanasosholaiti mwenye umri wa miaka 28.

Iliripotiwa kuwa aliaga dunia Ijumaa asubuhi, Oktoba 7, 2022. Ingawa, haijulikani ni nini kilisababisha matatizo hayo, inasemekana alikata roho wakati akifanyiwa upasuaji hospitalini.

Katika video iliyorekodiwa muda mfupi baada ya kufa, daktari alisikika akimwomba msamaha.

Kifo chake kinatokea siku chache tu baada ya mwanasosholaiti kutoka Kenya Vera Sidika kusimulia kwamba alinusurika kifo kutokana na upasuaji wake wa kuongeza makalio.

Vera alipakia picha akiwa bila makalio yake makubwa na kusema kwamba ilimlazimu kufanya upasuaji mwingine wa kuyapunguza baada ya upasuaji wa awali kuyaongeza kumletea matatizo ya kiafya amabyo kulingana na yeye nusra yamsafirishe jongomeo.

Nchini Kenya, baadhi ya wanadada ambao wameweka wazi kuwa wamewahi fanyiwa upasuaji kama huo wa Liposuction ni pamoja na mwanasosholaiti Lady Risper pamoja pia na mwanaYouTube Murigi Munyi almaarufu Yummy Mummy.