Mcheshi Daddie Marto atarajia mtoto wa tatu licha ya kupanga uzazi

Daddie Marto na mkewe wanamtarajia mtoto wao wa tatu sasa

Muhtasari

• Baba huyo wa watoto watatu na mwengine mtarajiwa alisema kuwa uja uzito huja kama tataizo kwa mkewe mpaka kiwango cha kulazwa hospitalini.

• Mke wake, Koku Lwanga alisema kuwa amekuwa akipigania afya yake baada ya kuwa mja mzito ila ako tayari kumpokea mwanawe.

Daddie Marto na mke wake Koku Lwanga

Mcheshi Daddie Marto amefichua kuwa yeye na mkewe wanatarajia mtoto wao wa tatu.

Marto alisema kuwa mkewe amehangaika sana wakati huu wa uja uzito na amekuwa mara nyingi hospitalini.

Alifichua kuwa hiyo ndiyo sababu ya kutangaza kutarajia mtoto bila furaha nyingi na hamu ya kuwajulisha mashabiki wao.

Baba huyo wa watoto wawili alisema kuwa mimba huja na changamoto nyingi kwa mkewe mpaka kiwango cha kulazwa hospitalini.

"Hii ndiyo sababu ya kutotangaza habari za matarajio yetu kama habari njema. Uja uzito huja kama jambo zito kwake na hata sasa yuko hospitalini kwa sababu mambo hayako shwari," Marto alisema.

Zaidi ya hayo, aliongeza kuwa ana matumaini kuwa mke wake atakuwa sawa na hata wakati wa kujifungua mwanao atakuwa kwenye hali nzuri.

Licha ya hayo mke wake Marto alikuwa mchangamfu na mwenye matumaini ya  kumaliza safari ya miezi tisa na kurejea nyumbani. 

Marto alisema kuwa yeye na mkewe watajikakamua kuwalea wanao ipasavyo wakisaidiana kwa majukumu ya ulezi.

"Tunatarajia mtoto wa tatu, mko upande upi? Hali ya kuwa mtu mzima na kuwa mzazi. Wueh! Lakini kama mnavyoona bado kuna uchangamfu kwa hivyo hiyo ni dalili ya kuwa ako sawa, tunaombea safari hii ," Marto alisema. 

Wawili hao walisema kuwa hawakuwa wamepanga kupata mtoto mwingine na walikuwa wametumia kila mbinu ya kupanga uzazi.

Mke wake, Koku Lwanga alisema kwamba amekuwa akipigania afya yake baada ya kuwa mja mzito ila yuko tayari kumpokea mwanawe.

Aliwafahamisha mashabiki wake hatua yake ya kunyamaza na kujiondoa mitandaoni akisema ni kutokana na anayopitia kwa sasa.

"Poleni kwa kunyamaza. Nimekua nikijaribu kuwa mkakamavu ili niweze kustahimili tatizo la kutapika kila mara na kukubali hali yangu ya kuwa mama kwa mara nyingine tena," Lwanga alisema huku akijibu ujumbe wa mumewe.

Licha ya kutumia njia za kupanga uzazi, Lwanga alisema bado alijikuta mja mzito.

Daddie Marto alisema kuwa mtoto wao mtarajiwa atakuwa mtoto wa aina yake kwani alipatikana licha ya matumizi ya njia za kupanga uzazi. 

Alisema kuwa hawana budi ila kukubali matokeo na kuyapokea kwa mikono miwili ili kujitayarisha kwa malezi.

"P2 ilimezwa,coil iliwekwa. Lazima aje tupende tusipende," Marto alieleza.