Nimechumbiana na watu 3 tu kabla ya Brown Mauzo - Vera Sidika

Sidika alisema kuwa hakutaka kuchumbiana na mtu maarufu baada ya kutengana na Otile Brown.

Muhtasari

• Sidika alisema kuwa akiwa kwenye chuo kikuu cha Kenyatta ndipo alipokuwa kwenye uhusiano wake wa kwanza ambao ulikuwa wa dhamana.

• Sidika alisema alikutana na mume wake akiwa kwenye mahusiano na mtu mwengine huku Brown Mauzo pia akichumbiana na mtu mwengine.

Mwanasoshalaiti Vera Sidka alifunguka kuhusu watu wapenzi wake wa kitambo ambao alichumbiana nao kuwa kabla ya kuwa kwenye ndoa na Brown Mauzo.

Katika mahojiano na Radio Jambo, Sidika alisema  akiwa katika chuo kikuu cha Kenyatta ndipo alipokuwa kwenye uhusiano wake wa kwanza ambao ulikuwa wa dhamana.

Aliongeza kuwa akiwa kwenye uhusiano huo ndipo alipoanza kupanga uzazi kwa kudungwa sindano ya kupanga uzazi.Aliifichua kuwa njia ya kupanga uzazi aliyotumia iliongeza ukubwa wa makalio yake licha ya madai kuwa alifanyiwa upasuaji..

"Nikiwa shule ya Star of the Sea nilikuwa na makalio makubwa bado ila yaliweza kuongezeka baada ya sindano hizo za kupanga uzazi. Nilikuwa naona haya kuwa na makalio makubwa na hata kujificha," mwanasoshalaiti huyo alisema.

Katika mahojiano na mtangazaji wa Radio Jambo Massawe Japanni, Sidika pia alizungumzia kipindi alipokuwa akichumbiana na Otile Brown .

Alisema kuwa baada ya kuwa kwenye mahusiano na mwimbaji huyo na kutengana hatimaye, hakutaka tena kuchumbiana na mtu maarufu.

Sidika alisema alikutana na mume wake akiwa kwenye mahusiano na mtu mwengine huku Brown Mauzo pia akichumbiana na mtu mwengine.

Aliongeza kuwa walipatana baadaye wote wakiwa hawako kwenye mahusiano yoyote na ndipo urafiki wao ukaanza.

"Nimechumbiana na watu watatu tu kabla ya mume wangu.Tulikuwa na urafiki wa ukaribu kabla ya kuwa kwenye mahusiano na yeye. Tulikuwa  tunaongea usiku mzima na kuongea mambo ya kibinafsi yaliyokuwa yakitendeka kwenye maisha yetu. Pia tuliongelea wapenzi wetu wa kitambo," Sidika alifafanua walivyoanza uhusiano wao.

Mwanasosholaiti huyo alisema kuwa alipenda uhusiano wao wa kirafiki na hata sasa ambapo wapo kwenye ndoa.