Super dad!Karen Nyamu amlimbikizia sifa msanii Samidoh

Mwanasiasa huyo alimtambua msanii huyo kama 'super dad',kwani amekuwa naye kila wakati.

Muhtasari
  • Mwanasiasa huyo alimtambua msanii huyo kama 'super dad',kwani amekuwa naye kila wakati
  • Karen aliandika ujumbe huo baada ya msanii huyo kuwaaga mashabiki wake, huku akianza ziara yake ya muziki nchi za nje
Samidoh aambiwa anafanana na Nyamu
Samidoh aambiwa anafanana na Nyamu
Image: Instagram

Karen Nyamu kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amemlimbikizia sifa baba wa watoto wake na msanii wa nyimbo za Mugithi Samidoh.

Mwanasiasa huyo alikuwa anamtakia kila la kheri Samidoh anapoanza ziara yake ya muziki.

Karen alimtambua msanii huyo kama 'super dad',kwani amekuwa naye kila wakati.

Karen aliandika ujumbe huo baada ya msanii huyo kuwaaga mashabiki wake, huku akianza ziara yake ya muziki nchi za nje.

Alimtakia kila la kheri katika ziara yake, huku akidai kwamba wanawe watampeza sana.

"Maskini watoto watampeza baba yao sana, kuwa na ziara yenye mafanikio,barikiwa na ufurahie baba watoto," Aliandika Karen.

Baadhi ya wanamitandao wamekuwa wakiwapongeza wawili hao na kudai huenda wakarudiana kutokana na uhusiano wao wa awali.

Wawili hao waligonga vichwa vya habari baada ya Karen kufichua kuwa Samidoh ndiye baba wa watoto wake