Bibi Harusi atemwa baada ya bwana harusi kugundua ana watoto 4

Mwanamke huyu alikuwa na watoto 4 kwenye ndoa ya hapo awali, habari ambayo hakumwambia mumewe mtarajiwa

Muhtasari

• Mwanamke alijitupa miguuni mwa mwanaume huyo akiomba amsamehe kwa kutomtaarifu kuwa alikuwa na watoto 4 na bado anampenda.

Siku ya maharusi wakifunga pingu za maisha huwa siku yenye bashasha na nderemo nyingi kusherekea wanapoingia maisha mengine.. Siku hii huwa yenye kupangwa ikapangika.

Ila kunayo harusi humo nchini Nigeria ambayo ilisherehekewa kwa vilio na majuto ya mjukuu, baada ya bibi harusi kuonekana akilia kwa nguvu huku wanawake wenzake wakijaribu kumliwaza.

Kizazaa hiki kilijili kwenye barabara kuu na watu walipoulizwa kinachoendelea, bwana harusi alisema:

''Bibi harusi hakuniambia, tayari ana watoto wanne kwenye ndoa ya hapo awali" 

Klipu hiyo iliwafanya walioitazama kumpa pole  Bi. harusi kwa jinsi ambavyo mwanamke huyo alijitupa miguuni mwa bwanake mtarajiwa kumhimiza asimwache lakini ombi lake likagonga mwamba.

Ila wanamtandao wengi walisema mwanamke huyo hastahili kuonewa huruma kwa sababu halikuwa jambo la busara kuficha habari muhimu kama hiyo kutoka kwa mwanamume ambaye alitaka kuolewa naye.

 “Kwa nini asimwambie mwanamume kabla ya harusi.? Yeye ni mdanganyifu kwenye ndoa, lakini naomba Mungu amrehemu." mwanamitandao mmoja alisema.

"Mke angemwambia kabla ya harusi hiyo inamaanisha kuwa anamficha mengi na hiyo ni hatari." Mwanamitandao wa pili alisema.

''Kama hadithi ni ya kweli  sifai  kumlaumu kijana hata kidogo… Mbona hukumwambia hata siku moja. Jipe moyo lakini dada yangu'' Mwanamitandao mwingine alionesha kujali.

''Kama yeye sio mtu wa kufunguka...Hataona mwanamume yeyote wa kumuoa'' 

''Tafadhali dada yangu mwambie mumeo  hadithi yako yote ya maisha'' mwingine alimshauri.