"Upendo pekee hauwezi kudumisha uhusiano"Anerlisa Muigai atoa ushauri maalum kwa wanaume

"Wanawake huchoka kuambiwa, fanya hivi, lipia hii," alisema.

Muhtasari

•Anerlisa amesema ni sharti mwanaume awe tajiri  na awe na uwekezaji mwingi kabla ya kujaribu bahati yake kwa mwanamke anayejitegemea.

•"Wanawake huchoka kuambiwa, fanya hivi, lipia hii. Na maisha yanaendelea. Huwa wanagundua wanataka kuwa na mtu ambaye anaweza kuleta kitu mezani," 

Anerlisa Muigai
Image: Anerlisa Muigai/INSTAGRAM
 

Mjasiriamali Anerlisa Muigai ameweka wazi kuwa wanaume maskini hawana nafasi ya kuchumbiana naye na wanawake wengine wanaojitegemea.

Kupitia Instagram, amesema ni sharti mwanaume awe tajiri  na awe na uwekezaji mwingi kabla ya kujaribu bahati yake kwa mwanamke anayejitegemea.

"Si matusi kwa mwanamume yeyote lakini ikiwa unatafuta kuchumbiana au kufunga ndoa na mwanamke anayejitegemea, zingatia kuwa na pesa nyingi na uwekezaji unaofaa," alisema kwenye Instastori.

Binti huyo wa seneta wa Nakuru Tabitha Karanja alibainisha kuwa wanawake hawapendi wanaume wanaowategemea kifedha.

"Wanawake huchoka kuambiwa, fanya hivi, lipia hii. Na maisha yanaendelea. Huwa wanagundua wanataka kuwa na mtu ambaye anaweza kuleta kitu mezani," 

"Mapenzi pekee hayawezi kudumisha mahusiano"

Anerlisa ndiye binti pekee aliyesalia wa mwanzilishi wa Keroche Breweries Tabitha Karanja na mumewe Joseph Karanja.

Hapo awali aliwahi kuwa kwenye ndoa na Staa wa Bongo Ben Pol kabla ya kutengana takriban mwaka mmoja baada ya harusi. Wawili hao walifanya harusi mwezi Mei 2020 katika Kanisa Katoliki la St Gaspar lililopo Mbezi Beach, Tanzania, katika hafla iliyohudhuriwa na marafiki wa karibu na wanafamilia.

Mwezi uliopita Anerlisa alifichua kuwa talaka yake na Ben Pol ambayo iliwasilishwa na mwimbaji huyo imekamilika.

Mridhi huyo wa Keroche aliwashukuru mawakili wake kwa kuhakikisha kuwa mchakato wa talaka yake umekamilika.

"Niko huru rasmi. Haitakuwa sawa kutowatambua mawakili hawa wawili ambao walifanya kazi bila kuchoka kuhakikisha kwamba talaka inafanywa haraka na sio kusubiri kwa miaka. Hamza Jabir na Hosea Chamba, asanteni kwa kazi zenu na kwa kufanya kila kitu mlivyoombwa," alisema kwenye Instasori zake.

Aliendelea kufichua mazungumzo yake na mmoja wa mawakili wake kuthibitisha kuwa talaka hiyo imekamilika.

"Rasmi Anerlisa na Ben si mume na mke tena, talaka imetolewa leo jioni ya saa tisa. Hongera," ujumbe mmoja ulisoma.

Ben aliwasilisha ombi la talaka mahakamani miezi kadhaa baada ya kutengana na mfanyibiashara huyo  kwa misingi ya tofauti zisizoweza kusuluhishwa na sababu zingine ambazo hazikuwekwa wazi.