Mwanadada anaswa kwenye video akiweka chupi kwenye kitoweo jikoni

Wanamitandao walighadhabishwa na kitendo cha mwanadada huyo asiye na soni.

Muhtasari

• Mtoto mdongo alifukuzwa pindi tu alipomletea  bakuli na kuanza kukoroga mchuzi huo.

Wanamitandao wameonekana kukerwa na video ambayo inaonyesha mama mmoja  akivua chupi yake na kuiweka kwenye chakula kilichokuwa motoni. 

Mwanadada huyo ambaye tabia yake sio za kiistaarabu anaonekana hadharani akiwa nje akiandaa kitoweo kutumia jiko. Kisha anavua chupi yake na kuitia kwenye sufuria ya kitoweo kilichokuwa kikitokota na kuanza kukikoroga kwa haraka.

Kisha mwanamke huyo anafunika sufuria ya kitoheo na kukiacha kuchemke zaidi.

Mtoto mdongo alifukuzwa pindi tu alipomletea  bakuli na kuanza kukoroga mchuzi huo.

Video hiyo ambayo ilipakiwa kwenye mtandao wa Twitter na ambayo ni ya sekunde 59, iliwachafua roho wanamitandao wengi wakionekana kuapa kutowahi kula vyakula vya kibanda.

@Wattah17 alisema, "Sio jambo kubwa..."

@ KentAlpha aliwaza kuwa, ''Alafu ukuwe mgeni nyumbani kwa mwanadada huyo.''

@Land_Of_Kenya alisema, ''Unaweza pata hiyo chupi ilikuwa na vitu vya kahawia  hapo juu.''

@eric_lilies alisema hukua akimaka, ''Waongope hawa mabiti wa Yezebeli... Nilimwomba Mungu nisiwai kujikuta tena kuwapenda viumbe hawa.''

@freddyholysan1 alisema, ''Kwani hali chakula? kwani hana watoto ambao wanakula chakula?...''

@MiteiRober alisema, ''Wanawake wengi wana dhana hii potovu kuwa ukichanganya chakula na nguo zao za ndani hua inawatuliza wanaume.''