Vera azungumzia tarehe ya kujifungua, mipango ya mtoto wa tatu

"Ilifanyika tu. Tuligundua ukiwa na miezi minne," alisema.

Muhtasari

•Vera ameweka wazi kuwa atajifungua mtoto wa pili kwa njia ya upasuaji kama ilivyokuwa na mtoto wake wa kwanza.

•Vera pia alifichua kwamba yeye na mume wake Brown Mauzo hawakupanga ujauzito wa mtoto wao wa pili pamoja.

Image: INSTAGRAM// VERA SIDIKA

Mwanasoshalaiti na mjasiriamali maarufu Vera Sidika amefichua kwamba tayari amepanga siku ya kujifungua mtoto wake wa pili.

Vera ameweka wazi kuwa atajifungua mtoto wa pili kwa njia ya upasuaji kama ilivyokuwa na mtoto wake wa kwanza.

"Nimepanga tarehe ya upasuaji wa CS. Kama nilivyosema hapo awali napendelea CS. Hakuna Maumivu," alisema Jumatatu.

Mke huyo wa mwimbaji Brown Mauzo alikuwa akiwashirikisha wafuasi wake katika kipindi  cha maswali na majibu kwenye mtandao wa Instagram.

Alipoulizwa kuhusu jinsia ya mtoto ambaye amebeba tumboni kwa sasa, mwanasoshalaiti huyo alidokeza kwamba pia yeye na mumewe hawajapata kutambua huku akiahidi kuandaa hafla kubwa  ya kufichua jinsia hivi karibuni.

"Itakuwa sherehe kubwa ya kufichua jinsia wakati huu. Siwezi kusubiri," alisema.

Vera pia alifichua kwamba yeye na mume wake Brown Mauzo hawakupanga ujauzito wa mtoto wao wa pili pamoja.

"Ilifanyika tu. Tuligundua ukiwa na miezi minne,

Aliweka wazi kuwa safari ya ujauzito wake wa pili imekuwa laini na hajakuwa akishuhudia dalili za ugonjwa wa asubuhi.

Pia alidokeza kuwa hana mpango wa kuongeza mtoto wa tatu wakati wowote hivi karibuni baada ya kujifungua.

"Labda nitaongeza mmoja tu baada ya miaka mitano," alisema.

Mwanasoshalaiti huyo pia alieleza kwamba sababu ya yeye kutoweka kwenye mitandao ya kijamii kwa muda ni kwa kuwa amekuwa akihusika katika utayarishaji wa kipindi Real Housewives of Nairobi.