Kuboresha mwili, kusafiri..;Vera afichua mipango yake baada ya kujifungua mtoto wa pili

Amedokeza kurejelea maisha ya uanasoshalaiti na kusafiri dunia baadaye mwaka huu.

Muhtasari

•Vera alidokeza kuwa anapanga kuboresha mwili wake na kusafiri kote duniani tena baada ya kujifungua mtoto wake wa pili.

•Vera alisifu janga la COVID 19 lililokumba dunia takriban miaka 3 kwa mafanikio yake katika kuanzisha familia.

Image: INSTAGRAM// VERA SIDIKA

Vera Sidika amedokeza mipango ya kurejea katika maisha ya uanasoshalaiti na kusafiri dunia baadaye mwaka huu.

Akizungumza kwenye ukurasa wake wa Instagram siku ya Jumatatu, mama huyo wa binti mmoja alidokeza kuwa anapanga kuboresha mwili wake na kusafiri kote duniani tena baada ya kujifungua mtoto wake wa pili.

Aidha, alionyesha fahari kubwa kwa maendeleo yake ya sasa na mafanikio katika kujenga familia.

"Miaka miwili iliyopita nimekuwa nikizingatia kujenga familia na ninafurahi kwamba hatimaye nilitulia na kuifanya," alisema.

Mwanasoshalaiti huyo mwenye umri wa miaka 33 alisifu janga la COVID 19 lililokumba dunia takriban miaka 3 kwa mafanikio yake katika kuanzisha familia huku akieleza kwamba lilimsaidia kutulia na kupata mchumba.

"Maisha yangu yamesawazishwa kikamilifu sasa. Asante Mungu. Kwa hivyo tunarudi kufanya miujiza. Jiandaeni wapenzi, inakaribia kuwa mbaya," alisema.

Vera alitangaza kuhusu ujauzito wake wa pili takriban wiki mbili zilizopita.

Katika tangazo lake, mama huyo wa binti mmoja alifichua kwamba amekuwa mjamzito kwa takriban miezi saba.

"Wapendwa, ndugu wa Asia yuko njiani!!!🎊💃🏼Mungu alikuwa na mipango ya familia yetu ndogo kukua zaidi 🙏  Tuliegundua tukiwa na miezi 4 na nusu," alisema.

Alifichua alikuwa akipanga kuenda nje ya nchi ili kufanyiwa upasuaji wa kuongeza matiti wakati alipogundua kuwa ni mjamzito.

"Ilinibidi kufuta safari yangu na kukumbatia muujiza wetu mdogo 😍🎊Nimejifunza kwamba kuwa mjamzito inamaanisha kuwa kila siku ni siku nyingine karibu na kukutana na mpenzi mwingine wa maisha yetu," alisema.

Kufuatia hilo, mwanasoshalaiti huyo alitoa shukrani za dhati kwa mumewe kwa kufanikisha ujauzito wa pili.

Aidha, alieleza furaha yake kubwa kuona kuwa bintiye mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi miwili atapata ndugu hivi karibuni.

"Nimefurahi sana kwamba Asia anapata ndugu ambaye atakua naye. BFF anakuja 💃🏼,"