Twitter yabadilisha nembo ya ndege wa buluu na kuweka ya mbwa

Musk hajazungumzia kuhusu mabadiliko hayo huku baadhi wakikisia kuwa ni utani wa siku ya wajinga ya Aprili mosi.

Muhtasari

• Akaunti rasmi ya Dogecoin ilitweet “Very currency. Lo! Sarafu nyingi. Jinsi Pesa. Kwa hivyo Crypto. Kwa majibu,”

Twitter yabadilisha nembo ya ndege wa buluu
Twitter yabadilisha nembo ya ndege wa buluu
Image: Maktaba

Twitter kwa mara nyingine imezua mjadala mkali baada ya nembo ya ndege kubadilishwa na taswira ya kichwa cha mbwa. Baadhi wanahisi kwamba mabadiliko hayo yanayoiga kichwa cha mbwa ni mzaha wa siku ya wajina ambayo huadhimishwa Aprili mosi kila mwaka.

Siku ya Jumatatu, watumiaji walibaini kuwa nembo ya ndege ya bluu kwenye ukurasa wa Twitter na skrini ya kupakia imebadilishwa na picha ya mbwaina aina ya shiba inu inayohusishwa na sarafu ya Dogecoin memecoin.

Kwa mtindo wa kawaida wa Musk, alituma meme akibainisha mabadiliko.

Katika meme hiyo, Musk alidokeza kwamba nembo ya ndege imepitwa na wakati na kuwa mabadiliko mapya ni watu kuanza kuzoea.

Akaunti rasmi ya Dogecoin ilitweet “Very currency. Lo! Sarafu nyingi. Jinsi Pesa. Kwa hivyo Crypto. Kwa majibu,”

Musk hajaelezea sababu ya mabadiliko hayo, lakini watumiaji wengine walidhani ilikusudiwa kuwa mzaha wa siku ya wajinga wa Aprili ambayo kampuni haikuweza kuleta kwa wakati mnamo Aprili 1.

Ilikuja siku chache baada ya Musk kuiomba mahakama nchini Marekani kutupilia mbali kesi iliyowasilishwa dhidi yake na wawekezaji wa Dogecoin ya $258bn kutokana na madai ya mpango wa piramidi, jarida la Guradian liliripoti.

Katika kubadilisha nembo ya Twitter, thamani ya Dogecoin iliruka kutoka US$0.079 hadi US$0.094, thamani ya juu zaidi ambayo sarafu imekuwa tangu Novemba mwaka jana.

Kulingana na memo ya ndani iliyovuja, Twitter sasa ina thamani ya chini ya US$20bn, chini ya nusu ya kile Musk alicholipa miezi sita iliyopita. Licha ya kuahidi kuondoa tiki za urithi za rangi ya buluu kwa watumiaji walioidhinishwa kuanzia tarehe 1 Aprili, tovuti hiyo imeondoa tu tiki kwenye akaunti kuu ya Twitter ya New York Times, jarida hilo liliripoti.

Twitter imepokea pingamizi kali kutoka kwa watu maarufu kwenye mtandao huo, baada ya kuwapokeza ujumbe wa kutaka walipie ada ili kuachiwa beji za buluu za kuonesha uhalali wa akaunti zao.