Hisia mseto baada ya Diamond kupatikana akicheza wimbo wa Harmonize nyumbani kwake

Diamond na watoto wake Tiffah na Nillan walifurahia wimbo 'Single Again' wakati wakicheza.

Muhtasari

•Katika video ambayo Diamond alichapisha, wimbo wa Harmonize 'Single Again' unaweza kusikika ukicheza kwa mbali

•Mashabiki wameendelea kutoa hisia mseto ikizingatiwa ugomvi mkubwa unaodhaniwa kuwepo kati ya wasanii hao.

katika siku za urafiki wao.
Harmonize na Diamond katika siku za urafiki wao.
Image: HISANI

Video inayomuonyesha staa wa Bongo Diamond Platnumz akicheza mchezo wa video na watoto wake, Tiffah Dangote na Prince Nillan huku wimbo wa Harmonize ‘Single Again’ ukicheza ndani ya nyumba yake imezua hisia kutoka kwa mashabiki.

Tiffah and Nillan walimtembelea baba yao siku ya Ijumaa na inaaminika dhumuni la ziara hiyo ni wapate kusherehekea Eid na familia yao ya Tanzania.

Ndani ya takriban siku mbili ambazo wamekuwa pamoja, Diamond amekuwa akionyesha baadhi ya nyakati zake nzuri na watoto hao wake na mwanasosholaiti wa Uganda Zari Hassan. Watatu hao wameonekana wakicheza pamoja, kujivinjari, kutazama filamu na hata kutembelea maeneo mbalimbali nchini Tanzania.

Katika video yao wakicheza mchezo wa video ambayo bosi huyo wa WCB alichapisha siku ya Jumamosi, wimbo wa Harmonize 'Single Again' unaweza kusikika ukicheza kwa mbali. Sauti ya mwanaume kwenye redio pia ilisikika.

Mashabiki wameendelea kutoa hisia mseto ikizingatiwa ugomvi mkubwa unaodhaniwa kuwepo kati ya wasanii hao wakubwa Bongo.

Haya baadhi ya maoni ya watumizi wa Instagram:-

neemababy_jr Kwani kuna ubaya gani akisiliza jameni

tomfoss_legend Hao walishapatana kitambo sana. Nyie ndo mnaojisumbuwa tu

sharifu5 Yaani mashabiki wa Hamo bado mnapendaga kuweka uadui wa Hamo na Mond wakati ni kijana wake

udom_blog Diamond hanaga ubaya na mtu

safi.kabemba.5 Kisha mimi nakataa kusikiliza nyimbi za Harmonize eti kisa mimi ni shabiki wa Diamond.

Mastaa hao wa Bongo ambao wameaminika kuzozana kwa miaka kadhaa sasa wameendelea kuwachanganya mashabiki wao kuhusu uhusiano wao halisi kutokana na matendo yao ya faragha na ya hadharani.

Hivi majuzi wawili hao walikutana uso kwa uso kwenye kikao cha chakula cha kufuturu jioni ya Jumamosi ya Aprili 15.

Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania aliandaa futari kubwa Jumamosi katika ikulu ya Dar es Salaam na kuwaalika watu mbali mbali wakiwemo viongozi wa serikali na wasanii wa miziki pamoja pia na waigizaji.

Baada ya futari hiyo ya Ramadani kukamilika vizuri Jumamosi jioni, kulizuka gumzo mitandaoni kuhusu wasanii hao wawili wanaodhaniwa kuwa maadui wasioweza kuonana jicho kwa jicho kukutana kwenye futari hiyo.