Baadhi ya kiki ambazo wanablogu hufanya ili kutafuta umaarufu.

Msanii Vivian na rapa Sosuun kupigana kwao pia ilikuwa tu kiki na namna ya kutafuta wafuasi.

Muhtasari

• Wanablogu wengi hupenda kufanya kiki ili kufuata wimbi wa umaarufu.

Image: INSTAGRAM// VERA SIDIKA

Wanablogu wengi hupenda kufanya kiki ili kufuata wimbi la umaarufu.

Kiki ambazo wanazifanya wanablogu hawa mara nyingi huhusiana na maisha yao ya kila siku.

Tumewaandalia Baadhi ya mambo ambayo wanablogu walifanya ili kutafuta umaarufu.

1: Dorea Chege

Katika video aliyopakia kwenye Instastory yake siku chache zilizopita alionekana bila mimba ila wiki baadaye alionekana akitomasa tumbo lake lililoonyesha ujauzito uliokomaa. Hii inaonyesha dhahiri kuwa alikuwa anatafuta umaarufu.

2: Sheryl Gabriela na Kabugi

Walikana kuwa katika uhusiano na kudai kuwa wao ni washirika wa biashara pekee. 

Ila kwa muda sasa umma ulifahamu kuwa wamekuwa wakichumbiana, kwa hivyo hii ina maana kuwa wanablogu hawa walikuwa wakitafuta umaarufu na kuchumbiana kwao ilikuwa kiki.

3: Mwanasosholaiti Amber Ray na mpenzi wake Kennedy Rapudo

Mwanasosholaiti Amber Ray na mpenzi wake Kennedy Rapudo kuwachana. Amber Ray na Rapudo walitupiana maneno kwa njia za mafumbo mitandaoni huku kila mmoja akizifuta picha za mwenzake mitandaoni.

Ila baada ya wiki tatu Amber Ray alipakia mfululizo wa picha za pamoja katika mwendelezo wa video akimtakia Rapudo 'kheir' njema ya siku ya kuzaliwa, hivyo kufutilia mbali uvumi wa kuachana ambao waliuanzisha wenyewe. Hivyo kuwachana kwao ilikuwa tu kiki.

4: Mwanasosholaiti mstaafu Vera Sidika.

Alitrend kwenye mitandao kutokana na madai ya kufanya upasuaji wa kupunguza makalio kwa kile alisema ni sababu za kiafya.

Msanii huyo mpya baada ya kuachia wimbo wake iligundulika kwamba alikuwa anatafuta kiki na ukweli ukabainika kuwa hakufanya upasuaji wa kupunguza makalio.

5: Msanii Vivian na rapa Sosuun

Kupigana kwao pia ilikuwa tu kiki na namna ya kutafuta wafuasi.

Kwani wawili hao walitayarisha wimbo pamoja na kuutoa hivyo bifu yao ilikuwa ya kutengeneza wimbi ambalo litawaongezea umaarufu kabla ya kutoa wimbo huo.

6: Mwanamitindo Manzi wa Kibera

Alipakia video kadhaa kwenye Instagram yake akiwa na gari jipya aina ya Prado TX miezi kadhaa baada ya kudai kwamba anaishi katika hali ya umaskini mkubwa licha ya umaarufu uliopitiliza.

Baada ya wiki mbili Manzi wa Kibera alisema kwamba gari hilo si lake na kudhihirisha kuwa ilikuwa kiki.

7: Willy Paul na Jovial

Kudai kuwa katika uhusiano wa kimapenzi ila ukweli ulikuwa kuwa walikuwa wanatafuta umaarufu kabla ya kutoa wimbo wao mpya. Kwani Jovial alisema kuwa hayuko katika uhusiano wa kimapenzi na Willy Paul.