(+video) Mchakato mzima wa jinsi Sidika alifanyiwa upasuaji wa kupunguza makalio

Video hiyo ilionyesha Sidika akiwa hospitalini kabla ya upasuaji

Muhtasari

• Sidika alisema kuwa alipitia vipimo vya afya kabla ya mchakato huo wa upasuaji wake kufanywa ili kuhakikisha kwamba ako tayari kufanyiwa upasuaji.

• Mke wa Brown Mauzo aliwashauri wanadada kuyatilia maanani anayosema na kujipenda kama walivyo ili baadaye wasipitie alichokipitia.

Image: VERA SIDIKA//INSTAGRAM

Mwanasosholaiti Vera Sidika ameweka video kwenye ukurasa wake wa Instagram inayoonyesha alivyojitayarisha kabla ya upasuaji wake.

Sidika alisema kuwa alipitia vipimo vya afya kabla ya mchakato huo wa upasuaji wake kufanywa ili kuhakikisha kwamba ako tayari kufanyiwa upasuaji.

Mama huyo wa mtoto mmoja hakuchapisha video yake ya upasuaji ila aliwaahidi mashabiki wake kuwa ataichapisha video hiyo Ijumaa.

"Nyaya nyingi ambazo ziko kwenye kifua changu na mguu zinaitwa ECG ambazo ni vipimo vya moyo," alisema.

Sidika alisema kuwa hakuwa anajiweza wala kujiskia wakati wa upasuaji ila aliweza kumwongelesha daktari wake amchukulie video hiyo.

Alisema kuwa aliiweka video hiyo ili iwe somo kwa wanadada wengine wanaotaka kubadilisha mauombo yao.

Mke wa Brown Mauzo aliwashauri wanadada kuyatilia maanani anayosema na kujipenda kama walivyo ili baadaye wasipitie alichokipitia.

"Kama uko na uhai na afya njema, mshukuru Mungu. Usiichukulie hivi hivi,"aliwaambia wanamtandao wa kike.

Sidika alisema kuwa ameyaona mabadiliko hayo yake kama bahati na kuwa amepewa nafasi nyingine ya kuishi vyema na kujipenda alivyo na Mungu.

"Niliupoteza mwili wangu uliokuwa ukiwapunga na ambao mlikuwa mmezoea kuona lakini hakuna kinachonituliza sasa kama kuwa na uhai wangu," mwanasosholaiti huyo alisema.

Mjasirimali huyo pia amesema kuwa sababu yake ya kuwajulisha wanamitandao kilichotendekea umbo lake ni kuwa angetaka kuwatoa hamu wanadada ambao wanataka kufanyiwa upasuaji wa maumbo yao.

"Siko hapa kwa ajili yenu ama kuwapa nafasi ya kupiga kelele na kunifanya nihisi mimi sio mtu. Tunaishi na tutafanya makosa ambayo yatafanya tuelewe na tujifunze," alisema.

Mumewe Vera Sidika, Brown Mauzo alimwandikia mjasirimali huyo ujumbe ulioonyesha anavyomuunga mkono mkewe wakati huu mgumu.

Mauzo alisema kuwa anautamani mwili wa Sidika wa kitambo ila anapenda haiba ya mkewe na roho yake safi kuliko alivyokuwa akipenda mwili wake.

Msanii huyo alimwonyesha Sidika upendo na kusema kuwa atampenda kama alivyo mama huyo wa mtoto wake.

"Mke wangu, natambua hili halijakuwa rahisi kwako hata kamwe. Nimekuwa na wewe kwa wakati huu wote wa mchakato uliopitia na nimeona kuwa wewe ni mwanamke mvumilivu," alisema.

Alisema kuwa amefurahia mkewe kupata amani na kuweza kujikubali alivyo ingawa haikuwa rahisi kwake.

Mauzo pia alisema kuwa Sidika kujitokeza na kuwaelimisha wanadada huko mtandaoni kuhusu kuongeza viungo vyao ni tendo la kijasiri sana.

Wengi walishuku mabadiliko haya ya Sidika na kusema kuwa anatafuta kiki.